Mlipuko wa bomu waua watu mjini Benghazi, Libya

Mlipuko wa bomu waua watu mjini Benghazi, Libya

Casuist

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2014
Posts
1,189
Reaction score
2,971
Bomu lililotegwa ndani ya gari, limelipuka na kuwauwa watu kadhaa katika mji wa Benghazi, nchini Libya.

Waliouwawa wanasemekana kuwa wanaharakati wa kisiasa wanaofahamika na wanaohusishwa na Jemedari mmoja anayeongoza kampeini ya miaka miwili, dhidi ya wanamgambo wa Islamic State.

Mohammed Bou-qa-i-qis ameuwawa kwa pamoja na watu wengine wawili, huku wengine zaidi ya kumi wakijeruhiwa vibaya.

Amekuwa akiendesha kipindi cha kila siku cha Runinga huku akiahidi kuwaunga mkono wanaharakati wanaopinga kampeini za I-S, inayoongozwa na Jenerali Khalifa Hafter.

Usalama katikati mwa mji wa Benghazi umeimarika pakubwa, lakini mapigano viungani mwa mji huo, bado yanaendelea,

Maiti ya watu 10 ambao hawajulikani, ilipatikana siku ya Ijumaa, ikiwa inaonekana waliteswa hadi kufa.
 
Hii kitu ndio mana naona bora tujitoe ICC waliua ghadaf na bado hawashitakiwi akina sakorzy
 
Back
Top Bottom