Mlipuaji Kenya ni Mtanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mlipuaji Kenya ni Mtanzania?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Dec 23, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 23, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MTANZANIA amehusishwa na mlipuko wa bomu la kigaidi lililotokea jijini Nairobi nchini Kenya juzi, baada ya mtu aliyekufa kwa bomu hilo kukutwa na hati ya kusafiria ya Tanzania.

  Kutokana na hilo, Jeshi la Polisi nchini linafanya upelelezi juu ya maiti huyo anayedaiwa kuwa ni Mtanzania. Katika mlipuko huo watu watatu walikufa na wengine 41 kujeruhiwa.

  Akizungumza jana Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini, Kamishna wa Polisi, Robert Manumba alisema wanafanya upelelezi huo ili kutambua kama kweli kijana huyo, Albert Orlando ni raia wa Tanzania.

  Manumba alisema upelelezi wa awali unaonesha kuwa kijana huyo alikuwa akitoka Tanzania kupitia mpaka wa Kilimanjaro na alikutwa na hati ya kusafiria iliyotolewa nchini.

  “Katika tathmini ya kwanza, imefahamika kuwa kijana huyo alikutwa na hati ya kusafiria iliyotolewa nchini, lakini hatuna uhakika kama kweli ni raia wa Tanzania na hati yake ya kusafiria imetolewa nchini kihalali,” alisema Kamishna Manumba.

  Kwa mujibu wa upelelezi wa awali, kijana huyo anayedaiwa alitoka nchini kwenda Kenya, alihusika katika mlipuko uliotokea ndani ya basi la Kampala Coach lililokuwa likipakia abiria kwa ajili ya safari ya kwenda Kampala nchini Uganda.

  Mlipuko huo ulitokea baada ya kijana huyo kudondosha kifurushi kilichokuwa na bomu baada ya kugundua kuwa polisi wanakagua mizigo ya abiria wote kabla ya kuingia kwenye basi.

  Aidha, Manumba aliwatoa hofu Watanzania kuwa uhalifu wa kigaidi ni wa kimataifa, si wa Tanzania na ambao una mtandao mkubwa ambao mara nyingi huwa unawahusisha raia wa kigeni na kuwataka vijana wasirubuniwe kufanya vitendo hivyo ambavyo havina faida kwao.

  “Utafiti unaonesha kuwa tishio la uhalifu wa kigaidi katika nchi za Afrika Mashariki ni kubwa sana hivyo ni jukumu la wananchi kutoa taarifa Polisi pindi wanapokuwa na wasiwasi na mtu hasa raia wa kigeni,” alisema.

  Kwa mujibu wa taarifa za magazeti ya Kenya jana, Kamishna wa Polisi wa Kenya, Mathew Iteere alimhusisha kijana huyo na kundi la wapigaji wa Al Shabaab wa Somalia wanaohusishwa na mtandao wa kigaidi wa Al Qaeda na kwamba kijana huyo aliyefariki, inaonekana alichanganyikiwa wakati akifanyiwa ukaguzi kwenye mlango wa basi na kuamua kuliangusha bomu ambalo hatimaye lililipuka.

  Alisema polisi wanaamini kuwa shambulio hilo la kigaidi lilikuwa limelilenga Jiji la Kampala, Uganda.

  Katika hatua nyingine, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya Taifa ya Kenyatta, Dk. Charles Kabetu alisema jana kwamba walipokea majeruhi 39, ambao kati yao, 19 ni Wakenya.

  Wengine ni Waganda sita, Warundi watatu, Wasudan wawili na Watanzania watatu. Waliolazwa walikuwa saba, ambao ni Wakenya watano, Mganda na Msudan.
  source habari leo
   
 2. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #2
  Dec 23, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Tumuombe Mungu sana kwa sababu shetani ameamua kujidhihirisha wazi wazi....hii hali si hali hata kidogo....inatisha na kustua....watu wamekuwa mashetani sana...hawana hofu hata kidogo...si jambo la kawaida hili...hapa ninavyozungumza nina machungu sana kwa kweli...we acha tu....inasikitisha mtu kupoteza uhai wa wenzake wasio na hatia!!!!!!!!!!
   
Loading...