Mliowahi kuwapa mabinti mimba mkiwa bado kimaisha hamjajipanga mliwezaje kuvuka hatua hii

Mboka man

JF-Expert Member
Aug 22, 2020
478
1,638
Kila nikiungalia umri wangu naona unazidi kwenda na bado kimaisha sijajipanga vizuri haswa kiuchumi bado sijawa stable kuwa na kipato cha uhakika kuendesha familia.

Hivyo basi kwa wale wana nzengo ambao mliowahi kuwapa mabinti mimba ikiwa kimaisha bado hamkujipanga Hebu tuelezeni vizuri.

Mliwezaje kuvuka hatua hii baada ya kutia mimba wakati maisha hayajasimama na kimaisha familia wakati hamkuwa vizuri.
 
Linapokuja swala la kuanzisha familia linahitaji uwee umejipanga kama haujajipanga basi jipange

Mimi nakushauri, tafuta kazi yeyote ile ambayo kwa siku ukiwa unapokea buku 2 sio mbaya kwa mwezi una 60000 ndani ya miezi Sita una 360000

Kama unaishi nyumbani nenda kapange chumba cha 20,000 au 30000 cha umeme ndani ya miezi 6 unalipa 180000 alafu nunua godoro used 30,000 au 40,000 na Mashuka mawili ya kulalalia
Ya elfu 3 ya Kigoma na ndoo ya kuogea

Ukiyaweza hayo basi tia mimba
 
Mimi nina kaka yangu kipindi hana kazi alimpaga mimba binti mmoja hivi

Aliletwa nyumbani akahudumiwa mpaka anajifungua, mzee Aliwapa chumba cha njee wakae bure huku wanajipanga baada ya kupata kibarua broo walihama nyumbani wakaenda kujitegemea hivyo kama home wanakuelewa waambie wakuandalie mazingira mapema
 
As long as hutamlaza mtoto wa watu na njaa, basi you are good to go.

Ukisubiri uyapatie maisha unaweza kuja kupata watoto ukiwa mzee. Pia maisha hayako straight line kwa wote, kuna wengine watafanikiwa kufuata process kabla ya kuzaa na wengine ndio kama hivyo hamna namna zaidi ya kupinda pinda.
Unforgetable
 
Unajua waliwahi sema mtoto huja na baraka? So hata kama hujajipanga usijali.

Ule ni uongo bro.

Hua anakuja na stress na self doubts za kutosha. Anasababisha ujue kujinyima zaidi ya ulivyozoea ni nini, anasababisha uexplore kila option na kila option will be locked before your eyes.

Kliniki niliambiwa mama mtoto anachelewa kujifungua kwakua simfanyishi mazoezi ya kutembea so nimfanyishe mazoezi ili ashushe injini.

I was on my way to rock bottom so I figured ngoja nipate pesa ya kumzalishia ndiyo nianze kumtembeza. Plan ilifeli, alijifungua huku mfukoni nina elfu 6, nilinunua gauni elfu 4 iliyobaki nikanunua ndizi za elfu moja na nyingine ikawa nauli ya kwenda hospitali.

Hakukua na complications so mchana wake akaruhusiwa, unaweza panda dalaldala na kichanga cha siku moja? Kikakae kwenye foleni na joto la Dar?

Mfukoni nina 1200. Bro sababu pekee sikua natoa machozi ni ili kumuonyesha mama mtoto kwamba kila kitu kiko sawa asijali.

Nitasema kitu pia. Ile elfu 4 niliyonunulia gauni ni pesa ambayo ilinifanya nijione nimetumia kwa ajili ya mtu anayestahili, nilijisikia amani saaaaana kuspend ile elfu 4.

Nishamnunulia mama yake simu, nikasomesha, nikanunua simu na matumizi mengine lakini yote hayafikii thamani ya ile elfu nne. Amani yangu imekua kujua familia iko fine regardless ya ama nimeprovide ama la.

Juzi nimembatiza. Ningeattach picha ila network hainiruhusu.

Go for it you will figure out everything as u go on. Pia kuna ule usemi ya kwamba mtoto huja na baraka? Ni wa ukweli.
 
Yaani haya maisha haya kila mtu ana mazito yake. Linakuja suala la kuhitaji kuwa na familia lakini kila ukijiangalia unahisi bora huo msoto uupatao ukukute hivyo hivyo ukiwa mpweke bila ya mwingine lakini upande mwingine umri unayoyoma.

Kupata Mtoto bila kujipanga kimaisha ni hatari lakini kupata mke ambae hawezi kukuongezea kitu kichwani cha maana katika hayo maisha ni hatari zaidi ya sumu ya mamba
 
Linapokuja swala la kuanzisha familia linahitaji uwee umejipanga kama haujajipanga basi jipange

Mimi nakushauli tafuta kazi yeyote ile ambayo kwa siku ukiwa unapokea buku 2 sio mbaya kwa mwezi una 60000 ndani ya miezi Sita una 360000

Kama unaishi nyumbani nenda kapange chumba cha 20,000 au 30000 cha umeme ndani ya miezi 6 unalipa 180000 alafu nunua godoro used 30,000 au 40,000 na Mashuka mawili ya kulalalia
Ya elfu 3 ya kigoma na ndoo ya kuogea

Ukiyaweza hayo basi tia mimba
Ndio maana we jamaa unaongoza kulia lia kwene mapenzi
Hakuna shortcut kwenye masuala ya mapenzi we tafuta tu hela
 
Bora we ulitia mimba mi niliachiwa kichanga ghetto

We ni Nani usiteseke hivi vitu havina formula utajikuta uko pazuri we pambana tu

Sahivi nafurahi kila nikimuona my baby daughter na afya nzuri na sitooa kamwe asije teseka na kadhia za mama wa kambo na huyu anatosha, hakuna kuongeza tena

Vijana tumieni condom
 
Mmmh
 
Kila nikiungalia umri wangu naona unazidi kwenda na bado kimaisha sijajipanga vizuri haswa kiuchumi bado sijawa stable kuwa na kipato cha uhakika kuendesha familia.

Hivyo basi kwa wale wana nzengo ambao mliowahi kuwapa mabinti mimba ikiwa kimaisha bado hamkujipanga Hebu tuelezeni vizuri.

Mliwezaje kuvuka hatua hii baada ya kutia mimba wakati maisha hayajasimama na kimaisha familia wakati hamkuwa vizuri.
Mpe mimba Binti anayejiweza ambaye anataka sana mtoto atamtunza!!
 
Kila siku naona single mama wanaongezeka, Sasa najiuliza WANAOZAA NAO HUWA WANAPIMA KWANZA????? au UWEPO WA NGOMA IS OVERRATED!!!
Baadaya mtu akifa kwa ngoma,wanaoandika historian fupi ya marehemu ndio wanapata shida
 
Mimi na mwenzangu tuko chuo ,ana mimba, mimba mpaka inafikisha miezi nane,kwao hawajui,kwetu hawajui.
Tulivoona anakaribia jifungua ikabidi tujikaze turudi home asije tukarudi na mtoto wakadhani tumeiba,tukapita home mama akajua(upande wa kiumeni haishtui),ila. yeye alivoenda kwao aisee wale wazazi walizimia wote.
Sema nilimwoa yule shetani wa kike,sikumwacha.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom