Mliotamani chama kipya, jiungeni na ADC! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mliotamani chama kipya, jiungeni na ADC!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by DCONSCIOUS, Mar 4, 2012.

 1. DCONSCIOUS

  DCONSCIOUS JF-Expert Member

  #1
  Mar 4, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,272
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Kuna watu ambao siku zote walikuwa wanaombea kianzishwe chama kipya eti chadema hakiwezi kudumu na hakina uwezo wa kuwa chama cha siasa mmoja kati ya hao ni Mwandishi wa Raia mwema ambae aliandika karibu Makala tano hivi zote ni majungu dhidi ya chadema huku akitaka kianzishwe chama kipya.

  Japo kuwa lengo lao kuu la Anguko la chadema limeshindikana lakini lengo lao la kuanzishwa vyama vipya limetimia kwani kuna ADC na CCK nahisi wanaweza kwenda hata kugombea Uenyekiti au ukaitibu mkuu huko badala ya kila siku kuamkia kwenye mitandao nakuongea utumbo dhidi ya chadema kwani mmechelewa sana , kugundua kuwa chadema ni chama makini.
   
 2. L

  LUNYASI Senior Member

  #2
  Mar 4, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 160
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  Umeongea point tupu,naunga mkono hoja
   
 3. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #3
  Mar 4, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Nani kakwambia anguko la CHADEMA limeshindikana? Kuanguka kwa chama is a process, mwaka 1995 nani aliamini kuwa NCCR ya Mrema ingeangukia pua? Miaka michache iliyopita nani aliamini kuwa CUF itasambaratika?

  It is only a matter of time hasa pale kampuni litakapokataa kubadili uongozi wake wa juu waliojihakikishia kuwa wao ndio wamiliki wa kampuni la CHADEMA.
   
 4. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #4
  Mar 4, 2012
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,381
  Likes Received: 3,341
  Trophy Points: 280


  unataka tubadili uongozi wa juu ili tukuweke wewe?
   
 5. DCONSCIOUS

  DCONSCIOUS JF-Expert Member

  #5
  Mar 4, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,272
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Anae subiria chadema ianguke na mfananisha na Fisi anaye mfwata binadamu nyuma akisubiri mkono uanguke ili auokote kumbe kwa binanadamu ni mbwembwe za kutembea tu.
   
 6. M

  Molemo JF-Expert Member

  #6
  Mar 4, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Huyo mwandishi kanjanja anaitwa Mayage S. Mayage
   
 7. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #7
  Mar 4, 2012
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Wenye akili walikuwa wanajua NCCR na CUF wanakoelekea labda wewe tu.
   
 8. C

  Cupid 50mg Member

  #8
  Mar 4, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huy wa Raia Mwema ni mmoja ya waliopo kwenye pay roll ya Mafisadi.
   
 9. N

  Nambelema Member

  #9
  Mar 4, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Tuache ubishi usiokuwa wa maana tunatakiwa kurejea historia ya vyama vya upinzani Tanzania.Baada ya kuanzishwa mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1992 na hatimaye kufanyika kwa uchaguzi ulioshirikisha vyama vingi 1995 ni chama cha NCCR MAGEUZI kilichokua chama kikuu cha upinzani kwa kupata wabunge wengi na kura nyingi za Urais. Mwaka 2000 - 2005,2005-2010 Prof Lipumba alikiongozaa chama cha cuf kwa kupata kura nyingi za Urais na Wabunge wengi ktk Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mwaka 2010 Dr Slaa alikiongoza Chadema kupata kura nyingi za Urais na Wabunge wengi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.hoja ya msingi tokea kuanzishwa kwa vyama vingi kuna vyama vya upinzani vilikuwa na nguvu kubwa leo vimekufa,NCCR MAGEUZI ilikuwa na nguvu kubwa hadi kumkosesha usingizi Baba wa Taifa Jk Nyerere kuzunguka na kumpigia kampeni Ben mkapa ili CCM isianguke. Rais Msitafu Ben Mkapa alikiri hadharani kuwa CUF ilikuwa ikimnyima usingizi.Vyama vya upinzani vitaitisha Ccm kwa muda mfupi vinakufa na kuibuka chama kingine.Ccm itaiua Chadema na kuibua chama kingine chenye nguvu kati ya CCK au ADC.
   
 10. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #10
  Mar 4, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  ADC ni chama kilichokuja kurudisha matumaini ya Watanzania kuhusu mabadiliko ya nchi baada ya vyama vingine vyote vya Upinzani kushindwa kutimiza malengo ya kuwakomboa Watanzania.
  Karibuni ADC - Dira ya Mabadiliko, Mkombozi wa Kweli wa Watanzania.
   
 11. Rock City

  Rock City JF-Expert Member

  #11
  Mar 4, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 1,270
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  ADC, nini sera zake.
  Wapi makao yake makuu,
  Akina nani ndio viongozi wake wakuu,
  Je kimeshapata usajili wa kudumu,
  Nini DIRA ya ADC,
   
 12. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #12
  Mar 4, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  ADC ni chama cha kisiasa ambacho kimeshaomba kupatiwa usajili wa muda kwa sasa kinaongozwa na Mwenyekiti Mhe. Said Miraji na Katibu Mkuu Mhe. Kadawi Lucas Limbu.
  Kwa sasa sera za ADC, Malengo ya ADC, Itikadi ya ADC na hata Ofisi Kuu(makao makuu) havingeweza kuwekwa hadharani kwa sababu kinasubiri kupatiwa usajili.
   
 13. DCONSCIOUS

  DCONSCIOUS JF-Expert Member

  #13
  Mar 4, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,272
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  ADC nashindwa kukitofautisha na Babu wa Loriondo.
   
 14. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #14
  Mar 4, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Unaweza kuuficha ukweli lakini sio matokeo ya ukweli, nasikitika kwamba unakikataa kitu unachokielewa, ushahidi wa hili ni majibu yako na zaidi nimefurahi umefananisha ADC na BaBU wa Loliondo ambaye alikuja kuwapatia tiba wale walokata tamaa kwa maradhi waliyonayo. Tiba ya ADC uzuri wake ni endelevu na ya uhakika yenye kuponya kiukweli na inayowafuata wagonjwa walipo sio mgonjwa kuifuata.
   
 15. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #15
  Mar 4, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kifo cha CHADEMA hakiko mbali kama unavyoshawishika kuamini. Kuna uwezakano mkubwa CCM wakamsimamisha mtu anatakayeungwa mkono na kanisa kama EL au mwungine, Kanisa likishatoa support yake, CDM inarudi ilikotoka! 2. Kuna manung'uniko mengi juu ya uendeshwaji wa CDM kama chama, tumeshaanza kusikia na viongozi wengine wameshatengwa! Hilo ni time-bomb lazima lilipuke kabla 2015!
   
 16. PMNBuko

  PMNBuko JF-Expert Member

  #16
  Mar 4, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 971
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huu ni ujumbe murua kwa Mayage, kibaraka wa CCM! Mtoa hoja, naomba umwongezee dozi!
   
 17. d

  dav22 JF-Expert Member

  #17
  Mar 4, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 1,902
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  waende vipi na ni waroho wa madaraka ambao wanapend akwenda kwenye chama kilichopo madarakani
   
 18. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #18
  Mar 4, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,696
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  "Just because all the swans in the swamp are black, it doesnt mean there are no blacks" - Prof Neil Ferguson.
   
 19. DCONSCIOUS

  DCONSCIOUS JF-Expert Member

  #19
  Mar 4, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,272
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Nakumbuka Mashekh walisema wataomba dua ya kuilaani chadema nilicheka sana kwani wewe na hao viongozi wako bado hamjajitambua kwa kuongea msivyo vijua.
   
 20. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #20
  Mar 4, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  ADC yenu ni wimbo ule ule wa CUF kwenye majukwaa tofauti

  Mtangoja CDM ife haitawezekana ila sifa zake ndyo zinazidi kusambaa hadi vijijini hivi sasa Kijiji cha Ipelele ambacho hakina hata diwani wa CDM sasa kimefanya uchaguzi wa viongozi wa CDM ngazi ya kijiji kumbukeni hawa hawajahamasishwa kama inavyo fanyika mjini.

  Hata mkilinganisha na NCCR au CUF sawa lakini kwa sasa ni zamu ya chama chenu kufa
   
Loading...