NANDERA
JF-Expert Member
- Mar 18, 2014
- 2,024
- 2,488
Naomba kuwauliza mliojenga Dar halafu nyumba zenu mmeweka madirisha yenye vioo, tena yanayofunguka upande mmoja kwa kusogeza na sioni kama mmefunga AC popote. Kwa jinsi kulivyo na joto mnapataje hewa hasa usiku mnapokuwa mmefunga madirisha? Kule milimani kutokana na baridi kali wanaweka madirisha ya vioo au ya mbao na juu ya dirisha huwa kuna vitobo vya kuingizia hewa.
Hapa Dar sioni nyumba nyingi zikiwa na hizi vents. Nia yangu si kuponda bali kujifunza maana natamani nyumba yangu iwe wazi isiwe hata na grills hewa iingie na kutoka kwa wingi wake lakini kutokana na changamoto za usalama haiwezekani.
Madirisha ya vioo ni fashion na yanapendeza ila sasa joto mnakabiliana nalo vipi? Mbadala ni upi?