Mliochaguliwa Kibaha Boys kidato cha tano

PATIENCE PB

Senior Member
Apr 3, 2014
163
37
4383c7f2c472ce36c5719d7580450298.jpg


Ilo ni bweni mojawapo la kidato cha tano hapo kibaha boys.
Kwanza nipende kuwapa pongezi sana kwa kuchaguliwa special school.Cha msingi mkifika hapo shule ni kuanza kusoma kwa bidii(msuli) kwa sababu ushindani uliopo pale ni mkali sana ....Usishangae ulikuwa unakimbiza(unaongoza) huko O level lakini ukafika pale ukashika mkia kama hautozingatia masomo.Kwa wewe unayetegemea kwamba umechaguliwa special school hivyo unategemea utawakuta special teachers ...sahau kuhusu ilo kwasababu pale school motto ni STRUGGLE FOR SUCCESS.... So itabidi u-struggle kweli kweli,japo walimu wapo watakachofanya ni kukusaidia jinsi ya kusoma na vitu gani usome.
Kuhusu suala la msosi,afadhali kidogo kwa wale ambao hawapendi DONA ...basi watafurahi kwa sababu mlo ni sembe .
Asanteni piteni hapa ili mfahamiane mapema
 
Walimu wa Kibaya boys...Kibaha girls na Tumbi sekondari zote zikiwa shule ndugu chini ya SHIRIKA LA ELIMU KIBAHA pia nao ni special teachers maana walimu wa shule hizi wanapatikana baada ya kupitia usaili wa kuandika na mahojiano wa sekretariati ya ajira....Kiujumla wapo vizuri vichwani tofauti na wale wengine wanaopangiwa vituo kisa wametoka vyuoni...Na muda wwte mwalimu anaweza tolewa kibaha boys kwenda Tumbi sekondari au Kibaha girls na kinyume chake....Na mishahara yao hawa jamaa ipo vzri
 
Back
Top Bottom