Mliobobea na Kutukuka katika ‘Critical Thinking ‘ kwa Kauli hii ya Spika Job Ndugai mmegundua nini Kinachokuja?

Huyu jamaa amesahau mkuu alichofanya wizara ya afya? Hatamtengua CAG ili aone mwisho wake
 
Kwamba kuna mtu anataka kufanya yake madudu ya kupiga mshiko lakini CAG ni kikwazo kikubwa
 
Shetani mkuu na mdogo wake wamekaliya misumari, walidhani CAG ni mtu wa ajabuajabu kama wao. Kinacho waudhi hawa washamba ni CAG kuibua hadharani wizi mkubwa wa mali ya watz. Hii tuhuma inawapa shida sana ukizingatia wanavyo penda sifa sana za kijinga. Watz tuko pamoja na CAG. Shetani na mdogo wake sasa ni muda wao na wao wanaisoma namba
 
Ndio maana wanasemaga uwongo hauna maisha marefu mkuu!!!
TUNAPIGWA KWELI KWELI SIO TULIPIGWA KWELI KWELI!!
 
Mku kwa uelewa wangu ninachokijua Assad hana kosa ndio report imepokelewa na wahusika.
Kama hawataifabyia kazi hiyo ripoti ndo tutajua ni nani mwenye mamlaka kati ya Spika na Rais kwani Assad ameshamaliza kazi yake.

Spika kumwambia ajiuzulu wakati ajua ripoti ipo mezani kwake ni kuwatuchanganya sisi Wananchi
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli wezi wamekaa kikao dhidi ya mlinzi wa kodi zetu(CAG). Na wametafuta mtu baradhuli wa kupiga kilele ili wenye akili ama busara kidogo tu wapime upepo unaenda je. Raia kwa wengi wao washaona CAG ndio mzalendo namba moja wa taifa hili na kwamba hana maneno ya kisiasa ya kuzuga ila anatembea katika njia nyembamba ya ukweli.
Sasa kazi imebaki kwa yule mkuu wa kaya anajipambanua kisiasa kuwa ndie mzalendo namba moja atakaa upande gani. Ama akae na genge linalojiita taasisisi ya uraisi linalomtuma spika kulinda ufisadi wao usiwekwe wazi au abaki na umma mkubwa uliojipambanua kukaa na CAG popote alipo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watueleze mbona siku hadi siku serikali I narudi nyuma kwenye compliance ya matumizi ya fedha? Wao wanashikilia issue ya dhaifu kuwa ndio itutoe kwa mstari. Waje na majibu isue ya kumwacha au kutoa CAG ni yao wao. Mbona wanatumbua tu kila siku safari hii wamekutana nampemba na sio Mchagga au msukuma wanakoma. Hawa hata kujilipua wanaweza
 
MSIGWA, tafadhal hebu tujuze kuhusu ili swala eti haujasikia fununu hapo ndani kwamba Baba mwenye hiyo nyumba nyeupe halali kutwa nzima anasonya kisa CAG?
Maana huku ndugai dhaifu anatuaminisha kuwa CAG anampa wakati mgumu jiwe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo kauli ndo inazidi kulionyesha kwamba bunge si tu ni dhaifu bali ni bunge bovu.
Kauli hii inamaanisha kwamba kabla ya kuja press conference alienda kwa Magu akampa maelekezo ni nini cha kuongea, yaani mkuu wa muhimili mmoja anaenda ku-seek instructions kutoka mkuu wa muhimili mwingine? Kama si kuwekwa kwapani ni nini?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama kuna sehemu walioandika katiba yetu walitenda haki kwa uadilifu mkubwa ni kwenye kipengele cha CAG. Waliona mbali sana. CAG is a very strong person as per kipengele hicho cha katiba. Kwa wapenda haki wote duniani, kazi anayoifanya CAG Assad ni ya kutukuzwa sana na ni mtu anayestahili kuombewa mno ili aendelee kurithisha uzalendo huu kwa vizazi vilivyopo na vijavyo katika nchi yetu. Mungu ambariki sana
 
Neno Bunge dhaifu alilenga serikali,akitaka bunge liiwajibishe serikali.
Akisema atarudia neno bunge dhaifu ni kuwaamusha wabunge kufanya kazi ya kuiwajibisha serikali kwa mahesabu mabovu yenye walakini nyingi.
Kama mlengwa ni serikali basi Magu atakuwa na wakati mgumu.Shortcut ni huyo mhasibu mkuu kuachia ngazi.Awapishe wafanye yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…