Mlioacha kazi na mambo yakagoma mtaani mlifanyaje?

Kwa uzoefu nilio/ninaopitia hakuna kwenda kuomba msamaha, unabadili mipango ya biashara kuwa rahisi zaidi kutekelezeka, unajishusha kufanya hata kazi za kupata buku 2 kwa siku huku ukiwa focused kutekeleza mawazo yako makubwa taratibu taratibu. Hebu mkuu kuwa FOCUSED na liwalo liwe lakini hakuna kurudi nyuma.

Utajiri unahitaji roho ngumu ndiyo maana matajiri ni wachache.
 
nimependa hio utajiri kuhitaji roho ngumu, ndio maana maboss wengi wana roho mbaya.
 
pambana mkuu,mimi mwaka wa 9 tangu nimetundika daluga,kuna kipindi mambo yanakaa sawa wakati mwingine yanadunda ile mbaya,sijatoboa bado ila naamini kuna sehemu nakosea na iko siku nitarekebisha na kusonga bila makwazo.....vyeti nilivitia moto ili hata nikikumvuka ajira nisiwe na reference....komaaa muzeeee
 
Kwa uzoefu nilio/ninaopitia hakuna kwenda kuomba msamaha, unabadili mipango ya biashara kuwa rahisi zaidi kutekelezeka, unajishusha kufanya hata kazi za kupata buku 2 kwa siku huku ukiwa focused kutekeleza mawazo yako makubwa taratibu taratibu. Hebu mkuu kuwa FOCUSED na liwalo liwe lakini hakuna kurudi nyuma.

Utajiri unahitaji roho ngumu ndiyo maana matajiri ni wachache.
Shukran ila kuna time unakuta akili inajutia maamuzi.
 
pambana mkuu,mimi mwaka wa 9 tangu nimetundika daluga,kuna kipindi mambo yanakaa sawa wakati mwingine yanadunda ile mbaya,sijatoboa bado ila naamini kuna sehemu nakosea na iko siku nitarekebisha na kusonga bila makwazo.....vyeti nilivitia moto ili hata nikikumvuka ajira nisiwe na reference....komaaa muzeeee
Tupo pamoja sana, nakutia moyo!
 
Tupo pamoja sana, nakutia moyo!
thanks mkuu,nilichogundua maisha yako controlled na mind set,pia wengi tunafeli kwa kutaka kujilinganisha na wakati ulipita au wanaokuzunguka,huku mtaani hela ipo ukiamua kubadilika na kuanza upya,wengi tunachagua cha kufanya na aibu zinatufunga tusione fursa.......
 
Life linaweza kukubana hadi ukatembea road kwenye baridi na ukahisi unaloana.... Usiache kazi kama huna straterg za biashara inayo eleweka.... Huku mtaani life ligumu balaa, kama huna roho ngumu kama ya Abu Bakr Al-Baghdadi Utakufa kiu katikati ya bahari....
 
Life linaweza kukubana hadi ukatembea road kwenye baridi na ukaloana.... Usiache kazi kama huna straterg za biashara inayo eleweka....

Utakufa kiu katikati ya bahari....
Ushauri mzuri sana. Pia watu wengi huacha kazi na kuamua kufanya kitu ambacho ameona tu mtu fulani anakifanya bila kujua ups and downs zake. Mwisho wa siku mtu unaangukia kichwa....
 
Unavyotoka kwenye kazi na kujitegemea changamoto haziwezi kukosekana lakini tambua nguvu iliyokusukuma kufanya mamuzi ya kuacha kazi hiyo hiyo itumie kukujenga katika uvumilivu na kutamani kufanikisha.
Kuna vitu vichachache huwa tunakosea
1. We over estimate the result but we under estimate the process, hilo tunafanya kosa kubwa maana process ni ngumu kuliko result/mafanikio

Easy come Easy Go
 
Back
Top Bottom