halfcastmangi
JF-Expert Member
- Apr 12, 2023
- 627
- 1,675
Habari wadau wa JF,
Kuna mlinzi kijana, mnene kiasi mweupe, mwanaume anaongea sana amegeuka ni kero kubwa kwa madereva, analazimisha rushwa hata kwa jambo dogo, gari ikiwa imebeba loose cargo hata mfuko mmoja ukiyumba anakufuata kwenye foleni na kuanza kukuchimba mkwara usiponipa hela naenda kukusemelea kwa meneja wa zamu upange mzigo wote upya, tena anaongezea meneja wa leo ni yule mdada ana kiburi utaona.
Usipo mpa anaenda mizani anasema hii gari mzigo umecheza wakati kikawaida loose cargo lazima kidogo mzigo ucheze lakini hauwi hatarishi, sasa kageuka kero sana anakusanya hela kama njugu na sio chini ya Tsh 5000.
Yaani kiufupi huyu mlinzi anaokota hela pale kuliko serikali, ana mambo mengi sana anayafanya pale, kuna muda unajiuliza hivi anashirikiana na uongozi au?
Serikali na vyombo husika tunaomba wekeni mtego mtamnasa tu anavyo okota rushwa haswa kuanzia saa 1 jioni.