TRA Kariakoo (Kipata/Lumunba) imekuwa kero kwa wenye magari madogo ya mizigo. Mamlaka imulike wafanyakazi wa pale waache hii tabia ya ovyo

Chukwu emeka

JF-Expert Member
Jan 12, 2018
23,410
36,559
Habari wanaJF,

Niende moja kwa moja kwenye hoja yangu, kumekuwa na usumbufu mkubwa wanaoupata madereva wa magari madogo katika eneo la Kariakoo, wanapokodiwa na Wafanyabiashara wanaonunua mizigo, pindi mzigo unapokamatwa kwa madai mbalimbali ikiwemo kukosa risiti inayojitosheleza,maofisa hao wa TRA wanalishikilia na gari iliyokamatwa na mzigo katika eneo lao bila kujali kuwa lile gari limekodiwa tu na halina tatizo.

Kuna baadhi ya magari yanakaa pale zaidi ya mwezi mzima huku wakiwa na majibu yasiyo na staa kwa watu wanaoenda kudai magari yao ili kuendelea na biashara.Madereva wanaonja joto la jiwe pale kwa majibu ya kejeli wakati wao (madereva) magari yao hayana tatizo lolote.

Dereva anakua hana kosa kwani yeye amepaki kwenye kituo chake cha kazi yeye hausiki na ukusanyaji wa mizigo .
Cha ajabu TRA wanakamata gari pamoja na mzigo na mara nyingi mwenye mzigo anakuwepo kwenye gari. Mzigo unapofikishwa TRA kwa madai kuwa risiti hazijitoshelezi maafisa wanagoma kuliruhusu gari licha ya kuwa mwenye mzigo wapo naye.

Japokuwa mzigo unakuwa si wa wizi na mmiliki wa mzigo yupo,bado imekuwa kero kubwa hata kwa wamiliki wakifuatilia magari yao wanapata majibu amabayo hayaridhishi wakati shida siyo gari ni mzigo ulio ndani na gari limekodiwa tu.

Madereva wanashindwa kupata hesabu za maboss wao na wenye magari wanapata hasara isiyo na sababu.

Waziri na wahusika ingilieni kati hili suala, magari yamejazana pale ofisini kwao wakati hayana hatia yoyote na mwenye mzigo anakuwepo.

Hii ni kero kubwa sana watumishi TRA Kariakoo wamulikwe inawezekana ni namna ya kutengeneza mazingira ya rushwa.

Mdogo wangu Mwigulu Nchemba tupia jicho kwa vijana wako
 
Mkuu hata mimi hapa nmetoka kwenye hio case kuna canter ipo pale na mzgo point yao wanasema wakiruhusu gari iende afu washushe mzigo hawapati wahusika, wafanyabiashara wanatelekeza mizigo/bidhaa zao inakua kero pale ofisin kwao.

Wanasema wakizuia gari na mzgo inasaidia wanapata wahusika/wauzaji

Tukirud kibinadamu wanazingua kwasababu kuna watu wanategemea kipato pale kama madereva.
 
Mara nyingi muhusika mwenye mzigo anakuwepo na anafahamika, mwenye gari anakosa gani na atafidiwaje kwa muda anaopotezewa
 
Unatakiwa wewe unaebeba mzigo ujiridhishe kwamba mzigo umelipiwa kodi zote stahiki.

Kubeba mzigo ambao hauna risiti zote na wewe unakua umekubali hatari ama risk inayotokana na kuubeba huo mzigo.

Ni sawa useme ubebe mtu na bangi ama cocaine halafu ukamatwe useme wakuachie gari yako waende na mwenye mzigo. Pale wote nyie ni wauza madawa ya kulevya. Maana yake unakua umesaidia mtu kutenda kosa, aiding and abetting.

Ili kuepuka kosa la aiding and abetting, hakikisha mzigo unaouchukua uko clear, sio magendo ama madawa ya kulevya maana TRA wakikukamata wanasema unasafirisha magendo ama mzigo usiolipiwa kodi inakua wewe huna cha kujitetea.

Hili liko wazi mkuu sio lazima usome PGO.
 
Utakuwa hujaelewa uzi vizuri, dereva anaendesha gari na mwenye mzigo yupo kwenye gari mambo ya risiti yanamuhusu nn? Dereva hakabidhiwi mzigo apeleke, ila anakuwa na mwenye mzigo na anayetolea maelezo siyo dereva ni mwenye mzigo
 
Unatakiwa wewe unaebeba mzigo ujiridhishe kwamba mzigo umelipiwa kodi zote stahiki.

Kubeba mzigo ambao hauna risiti zote na wewe unakua umekubali hatari ama risk inayotokana na kuubeba huo mzigo.

Ni sawa useme ubebe mtu na bangi ama cocaine halafu ukamatwe useme wakuachie gari yako waende na mwenye mzigo. Pale wote nyie ni wauza madawa ya kulevya. Maana yake unakua umesaidia mtu kutenda kosa, aiding and abetting.

Ili kuepuka kosa la aiding and abetting, hakikisha mzigo unaouchukua uko clear, sio magendo ama madawa ya kulevya maana TRA wakikukamata wanasema unasafirisha magendo ama mzigo usiolipiwa kodi inakua wewe huna cha kujitetea.

Hili liko wazi mkuu sio lazima usome PGO.
.
 
Mkuu hata mimi hapa nmetoka kwenye hio case kuna canter ipo pale na mzgo point yao wanasema wakiruhusu gari iende afu washushe mzigo hawapati wahusika, wafanyabiashara wanatelekeza mizigo/bidhaa zao inakua kero pale ofisin kwao.

Wanasema wakizuia gari na mzgo inasaidia wanapata wahusika/wauzaji

Tukirud kibinadamu wanazingua kwasababu kuna watu wanategemea kipato pale kama kwah
 
Mkuu hata mimi hapa nmetoka kwenye hio case kuna canter ipo pale na mzgo point yao wanasema wakiruhusu gari iende afu washushe mzigo hawapati wahusika, wafanyabiashara wanatelekeza mizigo/bidhaa zao inakua kero pale ofisin kwao.

Wanasema wakizuia gari na mzgo inasaidia wanapata wahusika/wauzaji

Tukirud kibinadamu wanazingua kwasababu kuna watu wanategemea kipato pale kama madereva.
Kwahiyo mtu akikodiwa na wakashika gari lake ndo mwenye mzigo anatokea???🤔🤔🙄🙄🙄Yaani TRA hawawezi kumpata so wanamtumia mwenye gari ndo amtafute??🤔🤔🙄
 
Unatakiwa wewe unaebeba mzigo ujiridhishe kwamba mzigo umelipiwa kodi zote stahiki.

Kubeba mzigo ambao hauna risiti zote na wewe unakua umekubali hatari ama risk inayotokana na kuubeba huo mzigo.

Ni sawa useme ubebe mtu na bangi ama cocaine halafu ukamatwe useme wakuachie gari yako waende na mwenye mzigo. Pale wote nyie ni wauza madawa ya kulevya. Maana yake unakua umesaidia mtu kutenda kosa, aiding and abetting.

Ili kuepuka kosa la aiding and abetting, hakikisha mzigo unaouchukua uko clear, sio magendo ama madawa ya kulevya maana TRA wakikukamata wanasema unasafirisha magendo ama mzigo usiolipiwa kodi inakua wewe huna cha kujitetea.

Hili liko wazi mkuu sio lazima usome PGO.
Sheria za kipumbavu kabisa, kila siku mbona watu wanakamatwa na madawa ndani ya ndege lakini ndege hazikamatwi, msafirishaji hana uwezo wa kujua kila mzigo una nini na umelipiwa au haujalipiwa TRA na sio kazi yake, na kama mwenye mzigo kakiri ni wa kwake tatizo liko wapi, ufanyaji kazi bila kutumia akili ndio huo
 
Back
Top Bottom