Mlinzi mwingine auawa Geita

Rwesiga

New Member
Nov 22, 2016
1
0
Mauaji ya walinzi mkoani Geita yamendelea kuwa tishio kwa usalama wao, baada ya mlinzi mwingine aliyetambulika kwa jina la Kisusi Iddy (40) mkazi wa Geita aliyekuwa akilinda maduka yapatayo 15 katika eneo la Mtaa wa Mwatulole kuuwawa kwa kupigwa na kitu chenye nca kali kichwani usiku wa kuamkia Januari Mosi mwaka huu.

Taarifa zilizopatikana eneo la tukio na kisha kuthibitishwa na Mwenyekiti wa Mtaa huo, Fikiri Toi zilieleza kuwa, baada ya waharifu hao kutekeleza mauaji hayo, hawakuchukua kituo chochote zaidi ya kutokomea kusikojulikana na kwamba mwili wa marehemu umekutwa ukiwa umefunikwa kwa shuka lake alilokuwa akilitumia rindoni nyakati za usiku likiwa limetapakaa damu pembezoni.

Kutokana na tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Geita, Mwalimu Herman Kapufi ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama, amefuta vibali vyote vya waganga wa wa tiba za asili kutokana na kudaiwa kuwa wao ni moja ya chanzo cha imani za Kishirikina zinazosababisha mauaji hayo na kwamba waganga wote wa tiba za asili wilayani Geita itabidi wasajiliwe upya.

Aidha akizungumza na waadishi wa habari ofisini kwake jana (leo Jumanne) Kapufi alisema kutokana na kukithiri kwa mauaji hayo, mamlaka yake inakusudia kufufua Jeshi la Jadi (Sungusungu) ili kusaidia kuthibiti mauji hayo.

Akifafanua kuhusu tukio hilo, Kapufi alisema uchunguzi wa awali ulionyesha kuwa wakati wa uhai wake, Kisusi Iddy alikuwa analinda maduka ya wafanyabiashara yanayofikia 15 na kwamba baada ya kufuatilia, imebainika kuwa hakuwa na mafunzo yoyote ya ulinzi.

Tukio hilo linatokea huku kukiwa na sintofahamu ya kutokuwepo kwa majibu sahihi ya chanzo cha mauaji hayo ambayo yamekuwa yakihusishwa na sababu kadhaa ikiwemo za ushirikina na ulinzi wa bila ya kuwa na mafunzo ya kukabiliana na waharifu.

Akizungumzia uamuzi uliochukuliwa na Mkuu wa Wilaya wa kufuta vibali vyote vya waganga hao, mdau wa maendeleo ambaye pia ni Mwenyekiti Chama cha Ualbino Mkoa wa Geita Isack Timoth, alisema uamuzi huo umekuja katika kipindi muafaka. "Nampongezasana Mkuu wetu wa Wilaya yetu kwa kufuta vibali vyaona mimi ninamuunga mkono kwani mbali na ukweli kwamba ramuli siyo kipimo sahihi cha kubaini ugonjwa, lakini wamekuwa wakiendelea kuitumia kwa wateja wao na haya mauaji ya walinzi yanasababishwa na wao. Alisema Timoth.

Mji wa Geita unazidi kukumbwa na matukio ya mauaji ya walinzi ambapo tangu mwaka 2014 hadi Januari Mosi mwaka huu Jumla ya walinzi 21 kati yao 15 wakiwa wa kampuni binafsi na sita wakiwa wakujitegemea wameuliwa kwa kuchinjwa.

Awali, Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Mponjoli Mwabulambo alisema wanaendelea na uchunguzi wa mauaji ya walinzi hao.
 
Huko nako, Leo wanaua albino, kesho wazee, keshokutwa Mawazo wa Chadema, siku nyingine wanaua walinzi, kuna siku tutasikia wamemuua mtoa Roho Ziraili
 
Asilimia 99.99 ya walinzi wote wanaouawa hawajapitia mafunzo ya Mgambo na wote wanauawa kwa kupigwa na vitu vyeye ncha kali au nyundo kwangu mimi watuhumiwa wa kwanza ni wamiliki wa Makampuni ya Ulinzi ambao wanaweza kuhusika ili watu waajiri walinzi toka kwao wa pili ni waganga wa kienyeji nje ya hao hakuna muuaji.
BADO MMOJA
TPX JIHADHALI TPX NAFUTIKA
 
Back
Top Bottom