Mlimani city 'si salama?'

Simba Mkali

JF-Expert Member
Jan 31, 2012
620
239
MLIMANI CITY 'SI SALAMA?'

Na Mwandishi Wetu

MAEGESHO ya magari mbele ya masoko ya Mlimani City yameelezwa kuwa 'si Salama'.

Habari zinaeleza kuwa hivi karibuni Prof. Kulikoyela Kahigi alivunjiwa kioo cha dirisha na kompyta yake ndogo kuibiwa. Naye Prof. Joseph Mbelle wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amewahi kuibiwa kompyuta yake ndogo kwenye maegesho hayohayo. Dirisha la gari lake wahusika kutokomea.
Juzi, Jumatatu ofisa mmoja alisema " Nilipaki gari langu tarehe 21 Febr. mwaka huu, nikaondoka na kuingia sokoni, nilikuta wamebomoa," aliezea ofisa huyo katika sauti ya huzuni " Niliporudi nilikuta kioo cha dirisha nyuma kimevunjwa na kompyta yangu imechukuliwa."
Amesema kuwa alipomweleza ndugu yake juu ya tukio hilo, alielezwa kuwa yeye si wa kwanza kuibiwa katika viwanja hivyo vya kuegesha magari.
Ofisa aliyeibiwa kompyuta yake alivyoliarifu tukio hilo kwa kampuni ya OMEGA Nitro inayofanya lindo katika eneo hilo,walisajili tukio hilo kwa Kumb. OB NO1763 kwa lindop la Mlimani City.
Aidha , walitoa OB No 684 kwa makao makuu yao yaliyopo Mikocheni Dar es salaam na kuahidi kuendelea na uchunguzi. OB ni kama RB za polisi wakati mtu anaporipoti shauri.
Aliyeibiwa kompyuta anasema alikuwa ameegesha gari "hatua chache" kutoka kwenye kichanja alipokuwa amekaa askari wa kampuni hiyo ya ulinzi.
Mkaguzi wa malindo wa OMEGA Nitro inayotokea Afrika Kusini alilifika kushuhudia jinsi wizi ulivyotokea.
"Cha kushangaza ni kwamba atafutwe askari aliyekuwa analinda eneo hilo, aliyekuwa kwenye kichanja pale juu: lakini walishindwa kumpata, eti hawamjui.
"Jambo hilo lilinipa mashaka kwa kuwa wizi unaotokea hapo una uhusiano wa moja kwa moja na walinzi wa kampuni iliyopata kandarasi ya kusimamia usalama wa wateja na mali zao." anasema.
Ofisa huyo anasema ni aibu kwa eneo la Mlimani City kutokuwa na kamera za usalamala (CCTV) za kusaidia lindo kwa kuonyesha kila tendo ndani ya maegesho.
"Nimeambiwa kila anayeibiwa huambiwa kuwa utawalawa eneo hauusiki na lindo la gari lake. Huu ni upuuzi," amesema akionyesha kulalamika.
"Wanakimbilia kuonyesha kadi kwa kuwa unapoingia na gari lako, unapewa kadi ambayo nyuma yake inaeleza kuwa usalama wa mali zako ni juu yako na kwamba unatakiwa kuondoa vitu vya thamani katika gari ulilopaki," anaeleza.
Ofisa huyo anakataa maelezo hayo akisema, " Kama hivyo, kwanini wanatoa kandarasi ya kuhakikisha usalama wa eneo lao?"..... SOURCE GAZETI LA MWANAHALISI - JUMATANO MACHI 21-27
 
Asante kwa taarifa simba mkali, binafsi nimekupata kwa uzuri.
 
Nchi hii bado ina safari ndefu kufikia utawala wa kisheria. Jamani, hata kama si rahisi kuiwajibisha kampuni ya ulinzi kwa upotevu wa vitu vya ndani ya magari, lakini ushahidi wa gari kuvunjwa vioo na walinzi wapo vichanjani mbona unatosha?
 
sasa hivi kilamahali ni si salama, hawa ni professional thieves, wanatumia electronic devices ku detect electronic items and gadgets, wanafungua magari kwa utaalam wa sensors na hata kuvunja vioo vya gari kwa kutumia fragile chemicals

tena hawa jamaa siku hizi wanatumia magari, wanatumia Toyota Noah, Escudo na pia corrolla limited, jumapili nasikia walikuwa Mahaba beach pale ununio, watu wanakula samaki na mitungi yao kumbe wajamaa wapo wamepaki gari yao busy wanafungua magari ya wateja, wamelamba vitu mbali mbali ndipo wakarupuka na kuwasha gari na kukimbia

sehemu yeyote sasa hivi yenye mkusanyiko mkubwa wa watu au shughuli usiache kitu cha thamani kwenye gari ulilopaki public
 
Ukishangaa ya Musa,,,,,,,,,,,,,,,,
Walinivunjia kadirisha kagogo ka nyuma ya gari wakakomba laptop
Amini usiamini kwa msaada wa walinzi sikuhiyo hiyo nikabidi niinunue tena laptop yangu mwenyewe, ile ile ilio ibiwa ikiwa haija futwa hata kitu kimoja
Hii ndio bongo zaidi ya uijuavyo
 
Mlimani si salama malalamiko ya aina hii ni mengi na hakuna hatua inayochukuliwa kwa ni ni hakuna hata kamera jamani ni aibu
 
Wana lalamika nini,kwa ninin waache laptop kwenye gari ambapo inaonekana?
 
mpaka waibiwe maprofesa ndo wanaona m.city sio salama, walalahoi wakiibiwa hakuna anayeripoti...
 
Only in Tanzania, mbona maduka kama haya kwao kuna ulinzi mzuri sana. tatizo la TZ askari mwizi, mkuu wa polisi mwizi, mkuu wa mkoa mwizi,waziri mwizi.... the list goes on mpaka kuchinang'anag'a
 
Haya ndo madhara ya kuruhusu maduka ya vifaa used. Mtu akikuibia kifaa kinaenda kuuzwa used madukani. Turuhusiwe kumiliki silaha kwa masharti nafuu tuwapunguze vibaka.
 
Hii mbona si habari mpya ndo wanagundua leo kuwa kuna uwizi Mlimani city?? tena siku hizi uwizi umepungua kwa sababu wateja washajua kuwa hapafai unless uwe mgeni au hujawahi kabisa kufika au hujawahi sikia habari za uwizi za pale.
 
na sio kuiba tu laptops.bali wanatoa kila kitu ndani ya gari.power window,taa,sidemirrow n.k.maeneo ya sinza,kijitonyama wezi wameshaniri.tujumuike kuwaua.
 
Hapo wenye magari tuwe tunaweka ulinzi binafsi. unaandaa watu kama wawili unawashusha mbali kidogo wanakuja kwa mguu na kuanza monitoring wakiwa mbali. Hapo pia unatakiwa kutegesha vitu vinakuwa kweupe ili kuwavutia. Naamini watanasa tu! Hapo ni kupiga mpaka kuua. Hata MZA mtaa wa Mza hotel karibu na Kuleana restaurant siyo salama walishaniliza printer mpyaaa! Walivunja lock ya mlango wa L/cruiser. Tujipange kuwaua hawa wanatutia umaskini sana!
 
Hapo wenye magari tuwe tunaweka ulinzi binafsi. unaandaa watu kama wawili unawashusha mbali kidogo wanakuja kwa mguu na kuanza monitoring wakiwa mbali. Hapo pia unatakiwa kutegesha vitu vinakuwa kweupe ili kuwavutia. Naamini watanasa tu! Hapo ni kupiga mpaka kuua. Hata MZA mtaa wa Mza hotel karibu na Kuleana restaurant siyo salama walishaniliza printer mpyaaa! Walivunja lock ya mlango wa L/cruiser. Tujipange kuwaua hawa wanatutia umaskini sana!

Nakubaliana nawe ktk bolded red,kusema tunawaachia tu polisisiem tutazidi kuingia umaskini. Well na tukifanya mara mbili tatu hivi kama hapo kwenye kijani nidhamu itarudi
 
mbona swala la wizi wa mlimani city imekuwa ni tabia-kila siku watu wanaibiwa-nashangaa hakuna hatua zozote zinazochukuliwa
 
Bora hao waliovunjiwa vioo na kuibiwa lap top, wengi wameibiwa magari yao pale mlimani city.
Inaonekana wizi pale ni jambo rahisi sana kutekelezeka ndio maana wezi hufanya pale ni shamba la bibi.
 
Afadhali hao wanaiba Laptop, mwaka 2011 jamaa yangu alipaki gari hapo mnakoita Mjini Mlimani alipotoka hakuliona, akaanza kulitafuta kwenye mifuko ya nguo zake, hajaliona mpaka kesho.
 
mara nyingi nikiwa nataka kwenda mlimani city napata tabu sana kujihakikishia usalama wa vitu ndani ya gari, kama niko full na laptop ya ofcn kwa kweli bora nihairishe iyo trip ya pale kama ni lazima sana ntabeba na gari natafuta parking chini ya vile vibanda vya wale jamaa tena kumuhaidi aniangalizie ntamtoa nikirud, na nikirud ndo nimpe buku etc lakini kama ni issue itanichukua mda labda dinner au kuchek movie napakigi gari kwa mshkaj maeneo ya sinza then naenda na tax na nikitoka nachukua tax naenda fata gari langu naishia! ni bora kulipa tax 8000/= kuliko kuibiwa laptop au kifaa cha gari na mwisho at least una peace of mind huku ukiendelea na kilichokupeleka!
 
Kilichobaki ni watu wote kuweka mgomo wa kutembelea eneo hilo hadi hapo wamiliki wa Mlimani City watakapotafunata ufumbuzi wa kudumu kuepusha wizi wa magari na mali za wateja. Mi nikiingia na gari yangu hapo laptop huwa nafungia nyuma ya buti ya gari kwa kweli huwa sina hofu sana otherwise huyu mkora aondoke na gari yote....Tukiamua tunaweza tatizo la watz kwa wale ambao hawajawahi kukumbwa na hayo matatizo ukiwaambia wagome ni wazi hawatakubali....
 
na sio kuiba tu laptops.bali wanatoa kila kitu ndani ya gari.power window,taa,sidemirrow n.k.maeneo ya sinza,kijitonyama wezi wameshaniri .tujumuike kuwaua.

Labda kuwaua economically. Tukifanya mgomo tukawacha kwenda pale watalazimika kuchukua hatua.
 
Back
Top Bottom