Mlimani city 'si salama?'

Nilichosoma hapa ni kwamba, wana JF humu ndani ni watu waliojaaliwa na mungu kupata elimu, kazi na maisha ya wastani. Yaani wana kazi nzuri, Magari, computer na vitu vingine vya maisha ya kisasa! Shopping zao ni sehem za quality za juu kama mlimani city! Lakini kwa kuwa wamezaliwa TZ badala ya kutumia nafasi zao vizuri kutoa mawazo yao kuleta mabadiliko zaidi kwa minds za watu wengine juu ya namna gani wao wamefanikiwa hadi kufikia hivyo kwenye mazingira haya magumu, wao wanatumia uelewa wao kutukana viongozi, kulaumu, kudai tu, kuchochea uhasama na mambo mengine meengi yasiyokuwa na tija!
 
Wana lalamika nini,kwa ninin waache laptop kwenye gari ambapo inaonekana?
Laptop yangu ni kama pete na kidole ,mpaka nimeota sugu begani kwa kuibeba,popote nilipo,niendapo ninayo kwa kwapa,asvali ninyang'anywe kwa nguvu kuliko kuibiwa
 
MKUU BAADA YA HAPO ULIFANYAJE? AU na wewe umeendeleza ukimya ili watu waendelee kuibiwa? Kwa nini baada ya kupata chako hujachukua hatua? Few days nilipaki pale nikaka garini. Dakika chache akaja mtu mwingine na kupaki gari ndani yake anakijana mwingine ambaye yeye alitoka akafungua mlango na kusimama nje ya gari. Kama nusu saa baadaye walikuja watu wengine 4 kwenye gari jingine wakablock lile gari la kwanza na kutoa bastola, yule kijana aliyekuwa nje akakimbia na kuungana na vijana wengine 3 walikuwa somefew meters toka kwenye gari. Huyo kijana akabanwa kumbe walikuwa wameiba gari mtaani wakakimbizwa na kuja kujificha pale. Ninachosema hapa ukimya wetu wanachangia kuendeleza dhuruma zilizopo hapa nchini na pia wezi ni kundi. Kimsingi kuna uwezekano askari wale wanahusika sana kuwalea na kuwakingia kifua na bila shaka wanagawana mawindo ya WIZI!
Ukishangaa ya Musa,,,,,,,,,,,,,,,,
Walinivunjia kadirisha kagogo ka nyuma ya gari wakakomba laptop
Amini usiamini kwa msaada wa walinzi sikuhiyo hiyo nikabidi niinunue tena laptop yangu mwenyewe, ile ile ilio ibiwa ikiwa haija futwa hata kitu kimoja
Hii ndio bongo zaidi ya uijuavyo
 
mara nyingi nikiwa nataka kwenda mlimani city napata tabu sana kujihakikishia usalama wa vitu ndani ya gari, kama niko full na laptop ya ofcn kwa kweli bora nihairishe iyo trip ya pale kama ni lazima sana ntabeba na gari natafuta parking chini ya vile vibanda vya wale jamaa tena kumuhaidi aniangalizie ntamtoa nikirud, na nikirud ndo nimpe buku etc lakini kama ni issue itanichukua mda labda dinner au kuchek movie napakigi gari kwa mshkaj maeneo ya sinza then naenda na tax na nikitoka nachukua tax naenda fata gari langu naishia! ni bora kulipa tax 8000/= kuliko kuibiwa laptop au kifaa cha gari na mwisho at least una peace of mind huku ukiendelea na kilichokupeleka!
 
MLIMANI CITY 'SI SALAMA?'

Na Mwandishi Wetu

hivi karibuni Prof. Kulikoyela Kahigi alivunjiwa kioo cha dirisha na kompyta yake ndogo kuibiwa. Naye Prof. Joseph Mbelle wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amewahi kuibiwa kompyuta yake ndogo kwenye maegesho hayohayo.
Jumatatu ofisa mmoja alisema " Nilipaki gari langu tarehe 21 Febr. mwaka huu, nikaondoka na kuingia sokoni, nilikuta wamebomoa," 27
Kuna Dr rutashamirwa naye alipaki merceds yake aliporudi akakuta hamna dirisha limebomolewa na iPad yake haipo sambamba na MacBook iliyokuwemo garini.
 
Laptop yangu ni kama pete na kidole ,mpaka nimeota sugu begani kwa kuibeba,popote nilipo,niendapo ninayo kwa kwapa,asvali ninyang'anywe kwa nguvu kuliko kuibiwa[/QUOTE...Mkuu utafiti wa hospitali ya Muhimbili inaonyesha kati ya wanaume wasiokuwa na uwezo wa kutungisha mimba wanawake wao ni wale wanaopendelea kubeba laptop mara kwa mara...be careful!!...
 
Back
Top Bottom