" Mlie, mpige kelele, mgalegale.. Mimi ndiye rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania. "

Nanoli

JF-Expert Member
Oct 15, 2015
3,735
5,970
Hili dongo c Kwan wananchi wa Dar pekee.. Kwa mtazamo wangu, ni dongo pia kwa Waziri nape aliyetangaza kuunda tume ya uchunguzi wa tukio hili la aibu. Magu anawaaibisha mawaziri wake na kuwajaza hofu ya kutojiamini katika maamuzi yao, kwenye dhamana waliyopewa. Kama wiki Jana akiwa kwenye mkutano wa chama pale Dodoma, alivyotamka kwamba.. "aliyekataza bunge kuonyeshwa live ni mimi " ni aibu kuwaweka mawaziri Kama kivuli huku akiendesha wizara zote Kwa akili yake na atakavyo.. Pia juzi tu, kamuaibisha waziri Mwakyembe siku ya pili tu baada ya kutangaza wasio na cheti cha kuzaliwa asioe wala kuolewa. Hii ni kuonyesha watanzania tumefeli kuongozwa na akili moja, huku bunge na mahakama vikiwa havina meno. Nakumbuka mahakama ililazimishwa ihukumu Kwa kupiga faini kesi zote ili kukusanya pesa za serikali. Pia Leo katika hotuba yake kawaeleza wananchi wa Dar.... "sishauriwi na mtu na sitaki kulazimishwa kufanya maamuzi"..hivi ni rais gani wa ajabu asiyetaka kushauriwa.. Sijapata kusikia rais asiyekua na mshauri.. Magu anatupeleka wapi, hii ni dalili ya kuomba poo nchi imemshinda, anajuta.. Anatibua maksudi ili uchaguzi ujao tusimchague... Nape dongo linakuhusu hilo.. Jiuzulu.
 
Back
Top Bottom