Mlevi aomba kazi kampuni ya bia(kituko).

Mlevi aomba kazi kampuni ya bia(kituko).

madaili

Member
Joined
Mar 6, 2014
Posts
32
Reaction score
27
Mlevi mmoja aliona tangazo la kazi kwenye kampuni moja ya bia, sharti lilikuwa ni moja tuu, awe mtaalam wa kunywa pombe, akatuma maombi ya kazi. Baadaye akaitwa kwenye usahili.
Siku ya usahili akawekewa glasi za bia tofauti tofauti kama kumi hivi. Alipomaliza kuonja bia zote, aliweza kusema aina ya bia, mwaka iliotengenezwa, kiwango cha alcohol na viwango vyote vinavyohusu kila bia iliyopo kwenye glasi. Wasahili wote wakabaki na butwaa. Meneja wa kiwanda akajifikiria kidogo, akamwita secretary wake akamnong'oneza kisha secretary akatoka, baada ya dakika chache akarudi na glasi imejaa nusu na akamkabidhi mlevi. Baada ya mlevi kunywa akasema "mwanamke, miaka 25, ana mimba ya miezi miwili" , baada ya hapo watu wote wakawa kimya kama jini limepita. Mlevi akahisi jamaa hawataki kumpa kazi, akasema hivi "Sasa kama hamnipi hii kazi nitasema mpaka jina la baba wa huyo mtoto", kabla hajamalizia kuongea wasahili wa kiume wote pamoja na meneja wakasema "umepita, umepita, kazi umepata bwana", halafu kila mmoja akatoka na kichwa ameinamisha chini.
Jumapili njema wanajamii
 
Pamoja na kuchanganua kwangu mambo kadha wa kadha hapa nimetoka kapa...!! Mweupe peee

BACK TANGANYIKA
 
Vipi kuhusu mwizi. Yeye akaombe kazi wapi??

Mwizi itabidi akaombe kazi benki, pesa ikiingia atajua ni ya magendo, feki na kama ni ya wizi atajua iliibiwa wapi na nani aliyeiba, unaonaje hapo?
 
Zaidi angepangwa kuwa mweka hazina kanisani ili zote pesa zisizo za haki azichambueee
 
Back
Top Bottom