Mlee Mtoto Wako; acha kumfuga

Mlee Mtoto Wako; acha kumfuga

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
34,100
Reaction score
79,501
MLEE MTOTO WAKO; ACHA KUMFUGA

Kwa Mkono wa, Robert Heriel

Katika jamii zetu za kiafrika imekuwa ngumu sana kutofautishaa kati ya Kufuga na kulea, yaani Ufugaji na Ulezi/Malezi.
Unaweza ukawa umezaa mtoto wako ukawa unamfuga kama kuku lakini wewe ukadhani unamlea, na unaweza ukadhani unamfuga mbwa lakini kumbe ukawa unamlea.

Ufugaji unahusu wanyama
Malezi yanawahusu wanadamu

Lakini Dunia ya sasa hasa jamii zetu, watu huwafuga watoto wao kama wanyama wakidhani kuwa wanawalea, na hii ni kutokana na kuwa wengi wetu sisi kama wazazi pia hatukulelewa bali tulifugwa tuu kama Paka au Mbwa. Pengine hili lisikufurahishe lakini huo ndio ukweli.

UFUGAJI ni kitendo cha kutunza wanyama na kuwapa chakula ukizingatia lishe bora, maji na sehemu nzuri ya kulala(zizi au boma). Ufugaji ni mojawapo ya shughuli mbalimbali za binadamu ambazo huweza kumuingizia kipato ambacho huchangia katika uchumi wa nchi. Pia uchumi huo huchangia katika maendeleo ya nchi fulani.

ULEZI/MALEZI ni mchakato wa maandalizi ya mtoto utakaomwezesha kukua, kukubalika na kushiriki katika shughuli za kijamii na kiutamaduni kwa kumlinda, kumjamiisha na kumpatia mahitaji na huduma za msingi.

Hii inatupa aina mbili za wazazi
1. MZAZI MFUGAJI
2. MZAZI MLEZI

Katika maana hizo tunaona kuwa Ufugaji na Malezi kuna ukaribu mkubwa wa kimuingiliano wa kimaana, sema tofauti iliyopo ni kuwa Ufugaji huhusu wanyama, na lengo kuu ni kujipatia kipato au faida, wakati MALEZI lengo lake kuu sio kujipatia kipato bali kumuandaa MAANDALIZI ya mtoto yatakayomsaidia mtoto(sio mimi au wewe mzazi) kukubali, kukabiliana na changamoto za maisha yake(sio maisha ya mzazi).

Kumlea mtoto sio kumpa tuu chakula, mavazi na sehemu ya kulala kwani hata Kufuga Kuku au mbuzi kuko hivyo hivyo. Kuna wazazi wanafikiri kuwa kumpa mtoto chakula ndio kumlea pekeake, jambo ambalo sio kweli, huko hakuna tofauti na kufuga.

Wazazi wengi ni wafugaji wa watoto badala ya kuwa walezi wa watoto. Na ukitaka kujua wewe ni mzazi mfugaji na sio Mlezi basi angalie lengo lako kuu la kumzaa mtoto au watoto.

Kama lengo lako kuu ni kujipatia faida hapo mbeleni basi jua tayari umeingia kwenye kundi la wafugaji na wala sio walezi.
Wafugaji ndio hufuga ili wajipatie faida hapo baadaye iwe faida ya maziwa, mayai, fedha au nyama.

Ndivyo alivyo Mzazi mfugaji, huyu humfuga mtoto kwa lengo la kujipatia faida hapo baadaye pindi atakapozeeka au atakapokuwa na uhitaji.

Mzazi mfugaji utamjua katika ufugaji wa watoto wake, kuanzia lugha, utoaji wa adhabu, na kuwaachia watoto wakishakuwa watu wazima.

Lugha inayotumiwa na wazazi wafugaji haina tofauti na mchungaji wa mbuzi akiwa machungani, imejawa na hasira, matusi, milunzi, mbinja, kurushiwa mawe kama sehemu ya kkupewa maelekezo.

Hujaona wazazi wanaowarushia mwiko watoto wao?
Hujaona wazazi wanao wamwagia watoto wao maji ati ndio hasira zao?
Hujaona wazazi wanaochapa watoto wao mpaka kuwajeruhi na kuwapa majeraha mazito?
Hujaona wazazi wanaoarushia mawe watoto wao?
Hujawaona wazazi kama hao?

Huko sio kulea bali ni kufuga mtoto.
Kitendo cha kumfuga mtoto wa binadamu kama mnyama kama sehemu ya malezi tulipe jina UFUGALEZI, Na wanaofanya kitendo hiko nimewaita WAFUGALEZI Maana yake watu wanaochanganya mbinu za ufugaji na malezi kumkuza mtoto.

Kumfuga mtoto ni kumfanya baadaye awe katili, aathirike Kisaikolojia,
Ndio maana unakuta hata humu mtandaoni(JF ikiwemo) mtu unaweza toa maoni yako lakini mtu akakutukana bila ya sababu, yaani ameathirika na Ufugalezi.

Au mwanaume anampiga mke wake hata bila sababu na kumjeruhi akidhani ndio anamfundisha adabu, hiyo yote ni madhara ya Ufugalezi. Na mara nyingi jamii za kifugaji ndio zimmeathirika zaidi na UFUGALEZI.

Adhabu apewzo Mbuzi, au kondoo ndizo apewazo binadamu. Jamani Binadamua anaakili na utashi sio mpaka umpige kikatili ndio aelewe, kumpiga haumsaidii bali unazidi kumpa matatizo, hasa ya kiakili na kitabia. Ni kumjengea tabia za kikatili.

Kama umeshawahi kuchunga mbuzi au kondoo, sio ajabu kumpigia mlunzi mbuzi aau kondoo, au kumrushia mawe ati ndio unamuonya asiende huko au asimame. Basi hali hiyo imepelekea hata kwenye kulea watoto usishangae mtoto akapigiwa mlunzi au kurushiwa mawe kama sio kunyoshewa fimbo ati ndio kumfundisha.

Hata shuleni Walimu wetu wengi hawakuwa walimu bali wafugaji waliotugeuza sisi mifugo yao. Unakuta mwalimu kasimama mbele ya darasa anafundisha akiwa amebeba fimbo hata nne mkononi kama mchungaji wa mbuzi. Alafu anajiita mwalimu, pumbavuu! Hamkuwa mnafundisha bali mlikuwa mnawatia watoto uoga wa kipuuzi.

Mtoto ni binadamu, anaakili, anaelewa, anajua pale unapomuelekeza kwa upendo na wala sio kwa chuki.

Kumlea mtoto ni kumuandaa mtoto na changamoto za maisha, sio kumlisha tuu ugali hapo na matembele ndio ukadhani umemaliza, huko ni kumfuga mtoto na kumfanya akutegemee siku zote za maisha yake.

Unakuta wazazi wengi wanadhana ya Mhe. Kishimba Mbunge wa Kahama Mjini kuwa watoto wanao wajibu wa kuwalipa fadhila wazazi, jambo ambalo sio kweli. Huo ni ufugaji wa watoto na wala sio kulea watoto.

Ukimfuga mtoto unamtengenezea mazingira ya kukuasi hapo baadaye kwani mtoto sio mnyama.

Ndio maana sishangazwi na malalamiko ya wazazi wa siku hizi wanaosema watoto wao hawawakumbuki wala kuwatunza,
Huwezi mfuga binadamu alafu akakukumbuka hata kidogo huo ndio ukweli.

Ukiona mtoto wako hakukumbuki basi jua kuwa ulikuwa unamfuga badala ya kumlea, hivyo umesabisha roho ya uasi na tabia ya kikatili kama ulivyomfanyia hapo zamani alipokuwa mdogo.

Kumbuka kama unadhani ulikuwa humfanyii ukatili, ndivyo naye anavyoona ni sawa tuu na wala sio ukatili kutokukuhudumia.

Kumlea mtoto ni kumpa Guideline ya mambo yaliyopo na yatakayokuja mbele yake.
Sasa mzazi hutaki kumuambia mtoto masuala ya mahusiano ya kimapenzi, masuala ya fedha, masuala ya dini, masuala ya mmarafiki, masuala ya kilimo, masuala ya usafiri, masuala ya kila aina, alafu unasema unamlea mtoto, huo sio ukweli huko ni kumfuga mtoto.

Mtoto lazima aambiwe na kufundishwa mambo yanayomhusu, yaliyopita, yaliyopo na yatakayokuja mbele yake sio kumdanganya danganya mtoto na kumtish kwa hadithi za kijinga na za kipuuzi.

Mtoto anapokuwa mkubwa na hukumpa muongozo akautafuta yeye mwenyewe hawezi kukuona tena kama mlezi bali atakuona kama Mzazi mfugaji. Huna utakachomuambia akakuelewa, pengine niseme atakuelewa kwa unafiki tuu.

Mathalani, unamdanganya mtoto kuwa asipokulea ukiwa mzee atapata laana, jambo ambalo ni uongo wa mchana kabisa ambao vijana wa siku hizi wanalijua, badala umfundishe mtoto upendo akupende wewe unamtishia kwa laana, vitisho vinaleta uasi.

Mtoto atachukulia mifano inayomzunguka kuwa mbona fulani hamsaidii mzazi wake na bado anafanikiwa, ataona ni uongo, alafu ataona wanaosaidia wazazi wao lakini hawafanikiwi licha ya kuwa wapo wanaofanikiwa. Mtoto ataona mbona ndugu yake wa damu(kaka) anakusaidia sana wewe kama mzazi lakini amemzidi kwa mbali kwa mafanikio. Mtoto atagundua kuwa unamtisha hakuna cha laana wala nini, bali akili za kipuuzi na vitisho vya wapumbavu.

Mtoto alelewe kwa upendo ili akikua arudishe Upendo kwako, sio umfuge kwa chuki alafu siku akikurudishia chuki umtishe kwa upuuzi wako.

Mzazi mfugaji utamuona siku Binti yake akiolewa, atataja mahari kubwa kwa vile anamchukulia binti yake kama ng'ombe au mbuzi.
Utasikia nimemsomesha, unaona nilivyomlisha amenona, toto toto, basi ilimradi auze mfugo wake.

Mahari itapangwa kulingana na binti alivyo kwa mfano
Mwenye degree na mzuri milioni tano
Mwenye diplomma na mzuri Milioni tatu
Aliyeishia kidato cha nne na mzuri milioni moja na nusu
Aliyeishia kidato cha nne wa kawaida laki tisa
Yaani Kama ng'ombe tuu.

Mzazi mlezi utamgundua pale binti yake anapoolewa, atataja kiasi cha kawaida kulingana na wakati na uwezo wa kijana anayekuja kuoa. Kama kijana atashindwa haitakuwa sababu, ataambiwa atoe nusu hiyo nyingine atamaliza. Mzazi mlezi atachukua mahari zinazolingana kwa kila binnti yake, kama ni milioni mbili basi wote mbili bila kujali mwenye degree wala aliyejaliwa uzuri.

Taikon nimemaliza.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Dar es salaam
 
Back
Top Bottom