Mlango wa Bombardier Q400 wazua kizaazaa baada ya kuruka

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
Abiria waliokuwa wakisafiri kwa ndege aina ya Bombardier Q400 ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kutoka Mwanza kuelekea Dar es salaam, walipata hofu baada ya ndege yao kuruka na muda mfupi baadaye kulazimika kutua tena katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza

Tukio hilo lilitokea jana saa 2.20 asubuhi uwanjani hapo, baada ya ndege hiyo kuruka kisha ikatua ndani ya dakika 20
Wakati ndege hiyo ikitua, Rubani aliwataarifu abiria kuwa wanalazimika kurejea uwanjani hapo kutokana na dharura iliyojitokeza

Wakizungumza kwa sharti la kutotaja majina yao gazetini, baadhi ya watumishi wa uwanja huo walisema walishangazwa na ndege hiyo kurejea muda mfupi baada ya kuruka, hali ambayo hutokea pindi ndege inapokuwa na hitilafu ya kiufundi

"Unajua ndege nyingi huanguka wakati wa kuruka na kutua, ndiyo maana jambo hili lilitisha abiria hata wafanyakazi.

"Lakini hakukuwa hitilafu kubwa ya hatari kwani baada ya kurejea na kukaguliwa, ilionekana mlango wa mizigo ya ndege hiyo ulifungwa vibaya, hivyo kuwasha taa ya tahadhari na Rubani kuamua kutua kwa dharura"alisema mmoja wa watumishi hao

Akielezea tukio hilo, mmoja wa abiria waliokuwa uwanjani hapo akitarajia kusafiri na ndege nyingine, alisema wakati ndege hiyo inatua kwa dharura, wafanyakazi wa uwanja huo walionekana kuchanganyikiwa

"Wafanyakazi walikuwa 'bize' mpaka tukashtuka, tulipouliza tukaambiwa ndege imeruka na kurudi kwa sababu imepata matatizo angani"alisema mfanyakazi huyo

"Ilipotua abiria wote waliteremka na wataalamu na mafundi wengine wakaanza kuikagua na mwishowe wakagundua mlango wa chumba cha mizigo ulikuwa haukufungwa vizuri

"Kwa hiyo, tatizo hilo waliteremsha na baadaye ndege iliondoka tena"alisema abiria huyo Wakati hao wakisema hayo, Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Mwanza, Easter Madale, alikiri kuwapo kwa tukio hilo ingawa alisema hakujua sababu zake

"Tukio hilo lipo, lakini siwezi kulizungumzia kwa sababu linawahusu watu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege

"Kwa hivyo nakuomba uwatafute hao kwasababu ndio wanaojua, ingawa linaonekana halikuwa tatizo kubwa kwani baada ya kutua, ilikaa muda mfupi na kuondoka tena", alisema

Chanzo : Mtanzania
 
Tuangalie jinsi mlango wa sehemu ya mizigo ya ndege aina ya Dash 8 Q400 unafanya kazi vipi na tatizo gani linaweza kuikumba kiusalama wa anga ndege hiyo kama mlango haujafungwa sawasawa :

Baggage Door Operation

Dash 8 Q400 Cargo and Passenger Door Operation 1


Source:Amelov Murat

How to do pre-flight inspection
airBaltic Bombardier Dash-8 Q400 external check by our pilots (part 2 of 6 )


Source: airBaltictraining



Description Bombardier Dash 8 Q400. Air Tanzania Bombardier Dash 8 Q400 is stretched to 78 passengers. Its 360 knot (667 km/h) cruise speed is 60–90 knots
 
Heee hata ki vitz changu kama mlango haujafungs sawa sawa kuna kitaa kinawaka ....kuashiria mlango iko wazi...
Itakua Bombadia pangaboi ? Au wamechukuliwa madereva wa bufalos zile hazina sign wala dash board ....wao huruka tu na kutua.
Bado sielewi kama mlango haujafunga na kama dashboard hainoshi hivyo pilot kuamua kuruka . Na jee huyo pilot hajalewa kweli, kama kuna mataa yaliwaka basi bila ya shaka kabla kuruka aliyaona. Otherwise technoligia ya 47
 
Back
Top Bottom