Mlalamikaji aangua kilio mbele ya tume

Benjamini Netanyahu

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
92,421
112,075

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Bonaventura Mushongi

MLALAMIKAJI Jimmy Sandy (60), ameangua kilio mbele ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), wakati akielezea jinsi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Bonaventura Mushongi na maofisa wenzake saba walivyoinyanyasa na kuidhalilisha familia yake.

Akitoa ushahidi dhidi ya malalamiko yake aliyoyafikisha mbele ya tume hiyo jana, Sandy alidai familia yake ilidhalilishwa kwa sababu ya kushindwa kuwapa polisi Sh 300,000 ambazo wafanyabiashara wa Pwani hutoa kwa kamanda wa polisi kwa ulinzi.

Shauri hilo linasikilizwa chini ya Mwenyekiti wa tume hiyo, Bahame Nyanduga.

Walalamikiwa ni Kamanda Mushongi, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Mkuranga, Edson Kasekwa, aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Japhary Ibrahim na aliyekuwa Mkuu wa Polisi Wilaya ya Mkuranga, OCD Mayenga Mapalala.

Wengine ni G.7429 Konstebo Swalehe, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Janeth Thobias, E.99272 D/Koplo Trano Peter na G.8941 Konstebo Nuhu.

Akitoa ushahidi wake, Sandy ambaye ni mmiliki wa kiwanda cha kutengeneza juisi aina ya Sophy, huku akiangua kilio alidai kuwa Juni 8, 2015 baadhi ya askari walifika nyumbani kwake Kiparang’anda, Mkuranga na kumkuta mkewe, wakataka awape fedha za ulinzi Sh 300,000 kwa madai wametumwa na OCD wa wilaya hiyo.

“Siku hiyo walikuja askari polisi wawili, wakajitambulisha kuwa ni Nuhu na Swalehe na kudai wametumwa na Mkuu wa Polisi Wilaya, waje wachukue Sh 300,000. Mke wangu aliwajibu sipo, waliondoka na kuacha namba zao ili niwasiliane nao,” alidai Sandy.

Sandy aliongeza kuwa walalamikiwa walidai utaratibu huo ni wa kawaida, kwamba wafanyabiashara wa Pwani hutoa kiasi hicho ili waweze kupewa ulinzi.

“Baada ya kupokea taarifa hizo kutoka kwa mke wangu, alinipa namba hiyo. Niliipiga na ilipokewa na mtu aliyejitambulisha kuwa ni Nuhu, nikamwambia siwezi kutoa kiasi hicho cha fedha,” alisema.

Pia alidai kuwa Juni 10, 2015, alipigiwa simu na dereva wake, Mohamed Ally ambaye alimweleza nyumbani kwake wamevamia askari kama 20 wakiwa na silaha.

Aliendelea kudai kuwa baada ya kuendelea kuhoji kilichotokea nyumbani na kama viongozi wa mtaa wake wapo, aliambiwa hawapo na afanye jitihada aiokoe familia yake kwani watoto, mke wake na wafanyakazi wake wa kiwandani wanateswa na polisi.

“Roho iliniuma sana siku hiyo kwa sababu aliyenipigia aliniambia nyumba yangu imegeuka bwawa la juisi, polisi wamechukua juisi yote iliyokuwa ikitengenezwa kiwandani kwangu na kuimwaga,” alidai Sandy.

Chanzo: Mtanzania
 
Simu za zaja na muda siyo mrefu kwa ninyi nyote mnaojifanya miungu watu was kuvunja sheria na kuamua mnachotaka ninyi kwa kuvunja katiba ya nchi pia.
 
Shauri hilo linasikilizwa chini ya Mwenyekiti wa tume hiyo, Bahame Nyanduga.

Walalamikiwa ni Kamanda Mushongi, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Mkuranga, Edson Kasekwa, aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Japhary Ibrahim na aliyekuwa Mkuu wa Polisi Wilaya ya Mkuranga, OCD Mayenga Mapalala.

Wengine ni G.7429 Konstebo Swalehe, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Janeth Thobias, E.99272 D/Koplo Trano Peter na G.8941 Konstebo Nuhu.

Akitoa ushahidi wake, Sandy ambaye ni mmiliki wa kiwanda cha kutengeneza juisi aina ya Sophy, huku akiangua kilio alidai kuwa Juni 8, 2015 baadhi ya askari walifika nyumbani kwake Kiparang’anda, Mkuranga na kumkuta mkewe, wakataka awape fedha za ulinzi Sh 300,000 kwa madai wametumwa na OCD wa wilaya hiyo.

“Siku hiyo walikuja askari polisi wawili, wakajitambulisha kuwa ni Nuhu na Swalehe na kudai wametumwa na Mkuu wa Polisi Wilaya, waje wachukue Sh 300,000. Mke wangu aliwajibu sipo, waliondoka na kuacha namba zao ili niwasiliane nao,” alidai Sandy.

Ndani ya Serikali hii inayojiita ya watumbua majipu?
Walikoswa wapi hawa askari mpaka Kesi imefikia kwa tume ya haki za Binadamu?
 
hakuna jipya...watahojiwa mwisho wa siku wataachwa kama walivyo
 
01dde425b7211e308d291be124e92612.jpg

Yaani Walikuwa wamezoea na kuona Kama ni haki yao.. Kula vya kunyonga
 
Dunia ya ajabu sana, huyo Jimmy hawezi kufanikiwa mpaka awe jirani na watoto wake alio watelekeza kwa mama tofauti tofauti.
 
Suala hili ni lazima serikali ilisimamie kwa dhati.Iwapo wafanyabiashara wanawachangia fedha makamanda wetu wa mikoa kila mwezi je raia wa kawaida atapataje haki yake katika vituo vyetu vya polisi? Hapo ni wazi iwapo mfanyabiashara amemdhulumu raia basi raia hawezi kupata haki yake katika vituo vyetu vya polisi kwani makamanda watakuwa wanakumbuka fadhila za kulipwa pesa kila mwezi. Jambo hili limetia doa jeshi letu la polisi na linatakiwa likemewe na jamii yote ili tubaki salama.Inauma sana mtu kupewa dhamana ya madaraka na kuwanyanyasa raia.Ingekuwa enzi ya baba wa taifa hao watuhumiwa wangesha achishwa kazi maana na fedheha kwa jeshi la polisi.
 
Kama wa pwani anachangiwa laki tatu he wa Dar nae angeamua kuchangiwa walau laki na kila mfanyabiashara ??? Hicho cheo kingependwa kuliko ikulu
 
Back
Top Bottom