Mkwasa, wote wataelewa tu, lugha yako ni rahisi

Lonestriker

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
640
241

attachment.php


Kufanikiwa kwenye mchezo maalum mara zote ni kitu cha kufurahisha na kuhamasisha, kufanikiwa kwenye michezo miwili ni kitu cha kipekee zaidi.

Shauku ya Wanigeria wengi ilikuwa ni juu ya uwepo wa kocha wao Sunday Oliseh kutaka kufahamu ataanza vipi kibarua chake. Wakati joto kwa upande wao likizidi kupanda, Watanzania kwa muda mrefu walikumbwa na sintofahamu juu ya lugha ngumu aliyokuwa akiizungumza Martinus Ignatus Maria Nooij, hakika muda uliokuwa umebaki haukutosha kumruhusu hata kuku kumeza punje ya mtama, tungeshuhudia nyasi za dimba la Taifa likiwaka moto.

Tunavyozungumza yamebaki kuwa historia, Charles Boniface Mkwasa 'Master' shujaa mpya aliyejua sintofahamu ya Watanzania na kuamua kutuliza moto uliotaka kuunguza Taifa kwa kuleta kile Watanzania walichokikosa kwa muda mrefu, lugha rahisi inayoeleweka.

Ukiangalia kikosi kilichoanza katika mchezo dhidi ya Tai wa Nigeria kilikuwa kimesheheni wanandinga ambao kila mfuatiliaji wa mpira Tanzania hakuwa na shaka wanastahili kuanza na mara tu kikosi kilipowekwa hadharani imani kubwa ilikuwa ni kushuhudia kazi ikitendeka.

Ndivyo ilivyokuwa, safu ya ulinzi ilikuwa bora kulinda, Nadir Haroub na Kelvin Yondan walikuwa matrafki wa ukweli kuzuia magari ya mkaa yasifike Ikulu. Yondani alidhihirisha ni kwa nini licha ya kutuhumiwa kuwa na nidhamu mbovu nje ya uwanja bado walinzi chipukizi wana kazi kubwa sana kumpora namba yake Stars.

Yondani alificha udhaifu wa Nadir Haroub na walinzi wa pembeni, Kapombe na Haji Mwinyi ambao kuna wakati walipitwa aidha kwa kuwa walikuwa wamepanda mbele kusaidia mashambulizi au kujipanga vibaya.

Hata hivyo bado Shomari Kapombe kwenye ubora wake alimtuliza Ahmed Mussa, yeye pamoja na Mwinyi Hajji walizitendea haki kamera za Azam Tv.

Katikati, Himid Mao alimpoteza kabisa Haruna Lukman kiasi cha kumlazimisha kocha Sunday Oliseh afanye mabadiliko dakika ya 36 tu ya mchezo kuokoa jahazi lake lisizame mbele ya Taifa Stars.

Ndani ya dakika 15 za kwanza tayari Taifa Stars ilionyesha hamu ya kutaka kumaliza ukame wa mabao, nafasi zilizotengenezwa na Mbwana Samata, Thomas Ulimwengu na Mrisho Ngassa bila kumsahau Farid Mussa zilikuwa ni mawingu ambayo yangeleta mvua kumaliza ukame.

Shujaa, Charles Boniface Mkwasa 'Master' alifanya mabadiliko ya akili sana, mbinu na nidhamu. Aligundua idara ya kiungo inahitaji mwanandinga atakayetengeneza nafasi na mwenye uwezo wa kupiga pasi za kupenyeza zenye mwendo, ndipo Said Ndemla alipoingia kuchukua nafasi ya Mudathir Yahya, ambaye alitimiza majukumu yake kipindi cha kwanza.

John Bocco alistahili kuingia ili kucheza mipira ya hewani, Mrisho Ngassa amecheza kwa kiwango cha juu isipokuwa hakuwa mzuri sana kwenye mipira ya hewani.

Farid Mussa winga hatari kwa sasa kwenye medani ya soka Tanzania alitoa msaada mkubwa sana pembeni. Hata hivyo uzoefu wake mchanga kwenye michuano ya kimataifa na pia kuonekana kuchoka kutokana na shughuli yake ya kupanda na kushuka kwenye wingi ya kushoto kulimfanya apumzishwe na Simon Msuva winga mwenye kasi kuchukua nafasi yake.

Sare ilistahili?

Kwa namna ambavyo mchezo ulivyokuwa na umakini wa hali ya juu hasa kwenye idara za ulinzi na kiungo za timu zote, Taifa Stars na The Super Eagles, sare ilistahili.

Pia, ubora wa walinda milango Ally Mustapha na mlinda mlango wa Nigeria, ni kielelezo cha ustahili wa matokeo yaliyotokea.

Changamoto kwenye safu ya ushambuliaji, inatengeneza nafasi nyingi lakini tatizo ni kuzibadilisha kuwa mabao. Kuna nafasi mbili za wazi kabisa ambazo zilitosha kutupa pointi tatu uwanjani.

Changamoto nyingine ni kwa mwanandinga Mwinyi Hajji, hufanya kazi kubwa lakini mwisho hushindwa kumalizia kazi yake nzuri hasa kupiga krosi zenye macho, bado mchanga nafikiri walimu wameliona hilo.

TFF, maamuzi ya kumpa timu Mkwasa ni ya busara, pongezi kwa Jamal Malinzi na sekretarieti yake. Mkwasa ameanza kutufundisha kwa kuzungumza lugha tamu, laini na inayopendwa na Watanzania waliokuwa na sintofahamu juu ya wapi walipokuwa wakielekea.

Rai ya SokaTanzania ni kwamba hamasa inahitajika zaidi, isiishie hapa. Mkwasa, hakika lugha yako itawafanya hata vipofu watamani kuiangalia Taifa Stars siku moja.

Chanzo: SokaTanzania
 

Attachments

  • Taifa_STARS_Facebook.jpg
    Taifa_STARS_Facebook.jpg
    409.3 KB · Views: 372
Mi sina wasiwasi na mkwassa kadri muda unavyokwenda ndio mambo yatazidi kuwa matamu, hongereni kwa mchezo mzuri, hata kama tumedroo..!!
 
Mi sina wasiwasi na mkwassa kadri muda unavyokwenda ndio mambo yatazidi kuwa matamu, hongereni kwa mchezo mzuri, hata kama tumedroo..!!

Mkwasa ni kama kasia la kitanzania linalosafiri kwenye bahari chafu ambayo boti zenye injini za wazungu zilionekana kushiindwa. Sare mbili moja ugenini dhidi ya Uganda na inayotusumbua kila siku na moja ya nyumbani dhidi ya Nigeria zimerudisha matumaini ya wengi.
 
Mimi siyo mshabiki wa soka na mambo ya soka kwangu ni hola, ila uandishi
wako umenivutia mno kwa nahau tamu eg "kuzuia gari la mkaa kwenda ikulu"
"muda mdogo usiowezesha kuku kumeza punje ya mtama" etc. Asante bro!
 
Mkwasa ni kama kasia la kitanzania linalosafiri kwenye bahari chafu ambayo boti zenye injini za wazungu zilionekana kushiindwa. Sare mbili moja ugenini dhidi ya Uganda na inayotusumbua kila siku na moja ya nyumbani dhidi ya Nigeria zimerudisha matumaini ya wengi.

Mkuu, hata mimi nimemkubali sana Kocha Mkwasa. Maana game ya jana tulicheza mpira mkubwa sana. Cha msingi afanyie kazi ufungaji mabao.
 
Mimi siyo mshabiki wa soka na mambo ya soka kwangu ni hola, ila uandishi
wako umenivutia mno kwa nahau tamu eg "kuzuia gari la mkaa kwenda ikulu"
"muda mdogo usiowezesha kuku kumeza punje ya mtama" etc. Asante bro!

Shukrani kwa kusoma.
 
Pamoja na kumsifia kote huko...

Taifa Stars ili iwe na uhakika wa kupenya inapaswa ishinde mechi zote zilizosalia...

Unahitaji walau points 10 na kuendelea kujihakikishia nafasi...

Kwa matokeo ya jana tayari naiona Misri ishapenya na nafasi inayogombewa ni hiyo ya pili...
 
Pamoja na kumsifia kote huko...

Taifa Stars ili iwe na uhakika wa kupenya inapaswa ishinde mechi zote zilizosalia...

Unahitaji walau points 10 na kuendelea kujihakikishia nafasi...

Kwa matokeo ya jana tayari naiona Misri ishapenya na nafasi inayogombewa ni hiyo ya pili...
Ni ngumu kufuzu but cha msingi team tunaiona inaimprove na sisi watanzania kurudisha matumaini na timu yetu
 
Hata kabla ya matokeo mabaya wengi tulijua kufuzu kwenye kundi lenye Nigeria na Misri ni ngumu sana. Lakini wengi tulitarajia kuona mpira ukichezwa, vijana wakiwatoa jasho hao Nigeria na Misri na sio kugawa pointi bure pamoja na kupata kapu la mabao. Tumekiona hicho kwa Mkwasa.
 
Back
Top Bottom