Mkwasa ateuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Yanga

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,621
8,411
Aliyejiuzulu nafasi ya Ukocha wa timu ya taifa ya Tanzania(Taifa Stars) Charles Boniface Mkwassa ameteuliwa kuwa katibu mkuu Yanga Afrika.

=======

Mkwasa aula Yanga, atoa neno

Klabu ya Yanga leo imemtangaza aliyewahi kuwa kocha wa klabu hiyo kabla ya kuwa kocha wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa kuwa Katibu Mkuu wake.
Mkwasa2.jpg

Boniface Mkwasa, Katibu mkuu Yanga Sc

Mkwasa anajaza nafasi iliyokuwa wazi kwa muda mrefu huku ikikaimiwa na Baraka Deusdedith baada ya kuondoka kwa Dkt. Jonas Jonas Tiboroha

Baada ya klabu ya Yanga kumtangaza Mkwasa kushika nafasi hiyo, mwenyewe amefunguka na kusema kuwa hana nia yoyote ya kurudi kwenye kiti kama kocha wa klabu hiyo kwani anadai anaamini walimu wote waliopo kwenye benchi la ufundi.

Mkwasa aliweka wazi msimamo huo mapema baada ya baadhi ya watu kuhisi huenda labda amekuja Yanga kuongeza nguvu katika benchi la ufundi

"Nimekuja Yanga SC kufanya muunganiko kati ya waalimu na Sekretarieti na pia sina nia yeyote ya kurudi kwenye kiti cha kufundisha kwenye klabu ya Yanga SC kwani sina shaka yeyote juu ya walimu waliopo kwenye benchi la ufundi" alisema Boniface Mkwasa Katibu mkuu Yanga SC
 
Kama hataingiliwa majukum ni jambo jema,anafahamu mpira anajua fitina na soka la bongo hivyo ni chaguo sahihi
 
Kina Omog& Lwandamila wanatoka kwao kuja kufundisha soka hapa,makocha wetu nini tatizo?
 
Mchezaji pekee wa zamani wa Bongo ambaye namuonaga hana njaa kama wenzie, ukimuacha Tenga.
 
Back
Top Bottom