Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,427
Matumizi ya dawa za kuongeza nguvu za kiume (mkuyati) yanazidi kutikisa nchini, huku baadhi ya mikoa dawa hizo zikiuzwa holela kwa wateja bila maelekezo ya daktari.
Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume Jumatano wiki hii lilitikisa Bunge, huku Naibu Waziri wa Afya, Dk Hamisi Kigwangalla akilazimika kutoa ufafanuzi wa sababu zinazochangia tatizo hilo.
Dk Kigwangalla alisema kiini cha tatizo hilo ni msongo wa mawazo na uchovu ambavyo hupoteza hamasa ya kufanya tendo la ndoa na kwamba, lazima mwanaume awe na afya njema kukabili tatizo hilo.
Akizungumzia hilo, Dk Kareem Segumba wa Hospitali ya Tanga Central Specialized Clinic ya jijini Tanga, anasema asilimia 80 ya watu wenye tatizo hilo, kiini chake ni mfadhaiko wa kisaikolojia.
“Kuna mambo mengi yamesababisha tatizo hilo, kubwa ni psychological (la kisaikolojia) zaidi. Ukiwa na mfadhaiko na msongo wa mawazo huwezi kufanya hilo tendo,” anasema.
Dk Segumba anataja sababu nyingine kuwa ni matumizi ya dawa za kulevya, unywaji pombe wa kupindukia, lishe duni, maradhi, kutofanya mazoezi na kupoteza hamu kutokana na kumzoea mwenza.
Aina za mkuyati
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini yapo makundi kadhaa ya dawa hizo, zikiwamo za vidonge zinazozalishwa viwandani na za vimiminika zilizowekwa katika vifungashio vya nailoni.
Kwa mujibu wa uchunguzi huo, vidonge vya viagra huuzwa kwa siri katika maduka ya dawa baridi kulingana na ubora na namna zinavyofanya kazi.
Mbali ya vidonge, ipo dawa iliyopo katika mfumo wa unga inayodaiwa kuingizwa nchini kwa njia za panya kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), ambayo huuzwa kati ya Sh2,000 na Sh4,000.
Dawa hiyo ya unga ambayo mwandishi aliiona, huchanganywa na lotion au mafuta na kisha kupakwa kwenye uume ikidaiwa huanza kazi baada ya dakika 30.
Mhudumu katika duka moja la dawa, alidai ingawa mkuyati ni kwa ajili ya wenye umri mkubwa kwa sasa vijana nao hutumia.
“Wateja wangu nawajua hata akija hapa akikuta mteja wa kawaida atasubiri mpaka tubaki mimi na yeye, anaweza kukwambia leo nataka ambayo nitakaa muda mrefu,” alieleza.
Naye Mwanasayansi bingwa aliyewahi kufanya kazi Hospitali ya Rufaa ya KCMC, Profesa Waitoky Nkya anasema dawa za kuongeza nguvu za kiume hazina madhara kama zikitolewa na madaktari.
Chanzo: Mwananchi