Mkuyati wawanasa vijana

Mkuyati wawanasa vijana

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,622
Reaction score
8,427
Matumizi ya dawa za kuongeza nguvu za kiume (mkuyati) yanazidi kutikisa nchini, huku baadhi ya mikoa dawa hizo zikiuzwa holela kwa wateja bila maelekezo ya daktari.

Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume Jumatano wiki hii lilitikisa Bunge, huku Naibu Waziri wa Afya, Dk Hamisi Kigwangalla akilazimika kutoa ufafanuzi wa sababu zinazochangia tatizo hilo.

Dk Kigwangalla alisema kiini cha tatizo hilo ni msongo wa mawazo na uchovu ambavyo hupoteza hamasa ya kufanya tendo la ndoa na kwamba, lazima mwanaume awe na afya njema kukabili tatizo hilo.

Akizungumzia hilo, Dk Kareem Segumba wa Hospitali ya Tanga Central Specialized Clinic ya jijini Tanga, anasema asilimia 80 ya watu wenye tatizo hilo, kiini chake ni mfadhaiko wa kisaikolojia.

“Kuna mambo mengi yamesababisha tatizo hilo, kubwa ni psychological (la kisaikolojia) zaidi. Ukiwa na mfadhaiko na msongo wa mawazo huwezi kufanya hilo tendo,” anasema.

Dk Segumba anataja sababu nyingine kuwa ni matumizi ya dawa za kulevya, unywaji pombe wa kupindukia, lishe duni, maradhi, kutofanya mazoezi na kupoteza hamu kutokana na kumzoea mwenza.



Aina za mkuyati

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini yapo makundi kadhaa ya dawa hizo, zikiwamo za vidonge zinazozalishwa viwandani na za vimiminika zilizowekwa katika vifungashio vya nailoni.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo, vidonge vya viagra huuzwa kwa siri katika maduka ya dawa baridi kulingana na ubora na namna zinavyofanya kazi.

Mbali ya vidonge, ipo dawa iliyopo katika mfumo wa unga inayodaiwa kuingizwa nchini kwa njia za panya kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), ambayo huuzwa kati ya Sh2,000 na Sh4,000.

Dawa hiyo ya unga ambayo mwandishi aliiona, huchanganywa na lotion au mafuta na kisha kupakwa kwenye uume ikidaiwa huanza kazi baada ya dakika 30.

Mhudumu katika duka moja la dawa, alidai ingawa mkuyati ni kwa ajili ya wenye umri mkubwa kwa sasa vijana nao hutumia.

“Wateja wangu nawajua hata akija hapa akikuta mteja wa kawaida atasubiri mpaka tubaki mimi na yeye, anaweza kukwambia leo nataka ambayo nitakaa muda mrefu,” alieleza.

Naye Mwanasayansi bingwa aliyewahi kufanya kazi Hospitali ya Rufaa ya KCMC, Profesa Waitoky Nkya anasema dawa za kuongeza nguvu za kiume hazina madhara kama zikitolewa na madaktari.

Chanzo: Mwananchi
 
usiseme unga ukiwa bara sema vumbi LA Kongo ukiwa pwani sema kasongo sebene.
 
Asante kwa taarifa

Sent From My iDevice using Jamii Forums Auto-reply Mobile App
 
usiseme unga ukiwa bara sema vumbi LA Kongo ukiwa pwani sema kasongo sebene.
hahaaa mna maneno nyie. eti kasongo. naamini mtu anakuwa machachari kama mpiga gitaa maarufu KASONGO!
mkuu @GENTAMYCIN tuwekee sawa kumbukumbu ya mpapasa nyuzi huyu.
 
Mmmh nguvu za kiume hivi lengo nini hasa yaani unywe mkuyati kumstarehesha mtu ,Si utafute mtu mnayefanana anayeridhika ,Mambo haya ndio yanarudisha watu nyuma kimawazo kwahiyo mtoto akizaliwa anaitwa Mkuyati au mundende khaaa,Haya maisha ni vituko
 
Matumizi ya dawa za kuongeza nguvu za kiume (mkuyati) yanazidi kutikisa nchini, huku baadhi ya mikoa dawa hizo zikiuzwa holela kwa wateja bila maelekezo ya daktari.

Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume Jumatano wiki hii lilitikisa Bunge, huku Naibu Waziri wa Afya, Dk Hamisi Kigwangalla akilazimika kutoa ufafanuzi wa sababu zinazochangia tatizo hilo.

Dk Kigwangalla alisema kiini cha tatizo hilo ni msongo wa mawazo na uchovu ambavyo hupoteza hamasa ya kufanya tendo la ndoa na kwamba, lazima mwanaume awe na afya njema kukabili tatizo hilo.

Akizungumzia hilo, Dk Kareem Segumba wa Hospitali ya Tanga Central Specialized Clinic ya jijini Tanga, anasema asilimia 80 ya watu wenye tatizo hilo, kiini chake ni mfadhaiko wa kisaikolojia.

“Kuna mambo mengi yamesababisha tatizo hilo, kubwa ni psychological (la kisaikolojia) zaidi. Ukiwa na mfadhaiko na msongo wa mawazo huwezi kufanya hilo tendo,” anasema.

Dk Segumba anataja sababu nyingine kuwa ni matumizi ya dawa za kulevya, unywaji pombe wa kupindukia, lishe duni, maradhi, kutofanya mazoezi na kupoteza hamu kutokana na kumzoea mwenza.



Aina za mkuyati

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini yapo makundi kadhaa ya dawa hizo, zikiwamo za vidonge zinazozalishwa viwandani na za vimiminika zilizowekwa katika vifungashio vya nailoni.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo, vidonge vya viagra huuzwa kwa siri katika maduka ya dawa baridi kulingana na ubora na namna zinavyofanya kazi.

Mbali ya vidonge, ipo dawa iliyopo katika mfumo wa unga inayodaiwa kuingizwa nchini kwa njia za panya kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), ambayo huuzwa kati ya Sh2,000 na Sh4,000.

Dawa hiyo ya unga ambayo mwandishi aliiona, huchanganywa na lotion au mafuta na kisha kupakwa kwenye uume ikidaiwa huanza kazi baada ya dakika 30.

Mhudumu katika duka moja la dawa, alidai ingawa mkuyati ni kwa ajili ya wenye umri mkubwa kwa sasa vijana nao hutumia.

“Wateja wangu nawajua hata akija hapa akikuta mteja wa kawaida atasubiri mpaka tubaki mimi na yeye, anaweza kukwambia leo nataka ambayo nitakaa muda mrefu,” alieleza.

Naye Mwanasayansi bingwa aliyewahi kufanya kazi Hospitali ya Rufaa ya KCMC, Profesa Waitoky Nkya anasema dawa za kuongeza nguvu za kiume hazina madhara kama zikitolewa na madaktari.

Chanzo: Mwananchi
vumbi la Congo tunauziea alfu 30..kichupa kidogo cha sindano

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmmh nguvu za kiume hivi lengo nini hasa yaani unywe mkuyati kumstarehesha mtu ,Si utafute mtu mnayefanana anayeridhika ,Mambo haya ndio yanarudisha watu nyuma kimawazo kwahiyo mtoto akizaliwa anaitwa Mkuyati au mundende khaaa,Haya maisha ni vituko


Mkuu:
Wewe hujui kitu kaa kimya.
Waache watu waingie kazini.
 
Mwanamke umpate kwa hela halafu tena utafute mkuyati hii ni shida au itakuwa wale wanaume wanaopenda kulelewa.Au ule wimbo wa mwanaume mashine ndo umewachanganya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jana nimetoka kuvunja chaga ... vumbi la Congo ni noma!!!!
 
hii itakuwaDar -es- salaam tu..huku hizi vumbi sjawai skia
 
Back
Top Bottom