Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hassan Bomboko amesema Watu 2 akiwemo Mwalimu Emmanuel Mbigili wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kulawiti mtoto

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,408
33,285
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hassan Bomboko (pichani kulia) amesema Watu wawili akiwemo Mwalimu Emmanuel Mbigili wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumlawiti Mwanafunzi wa awali katika Shule ya Mount Moriah na kumuharibu sehemu zake za siri ambapo taratibu za kisheria zikikamilika watafikishwa Mahakamani.

DC Bomboko (@hassan_bomboko) amesema hayo leo March 28,2024 alipofika katika Shule hiyo ili kufuatilia sakata hilo lilioibua hisia za Watu wengi mitandaoni wakiwemo Watu mashuhuri tangu pale Wazazi wa Mtoto huyo mwenye umri wa miaka sita walipojitokeza na kuelezea jinsi Mtoto wao alivyolawitiwa huku wakidai Muhusika ni Mwalimu wake, Emmanuel na wakilalamikia haki kutotendeka.

DC huyo amesema mwingine aliyekamatwa ni Mjomba wa Mtoto huyo aitwaye Benjamin Augustine ambaye anafanyiwa pia uchunguzi ili kubaini kama alikuwa anamfanyia pia vitendo hivyo Mtoto wakati akiwa nyumbani.

“Hili jalada lipo kwa Mwanasheria wa Serikali niwaombe sana Watanzania tuwe watulivu wakati Serikali inaendelea kuchukua hatua za ziada katika kukabiliana na matukio kama haya, jambo hili limegusa hisia za Watu wengi Wananchi walitaka kuona tamko la Serikali, niwahakikishie haki itapatikana”

#MillardAyoUPDATES

Pia soma:
- Mtoto adaiwa kulawitiwa na Mwalimu na kupewa biskuti na soda. Familia yaomba msaada
 
Ikithibitika pasina shaka,
wahusika wachukuliwe hatua kali sana za kisheria tena bila huruma, ili kusudi iwe fundisho kwa wengine waliopanga kufanya vitendo vya aibu, na wale wanaoshiriki vitendo hivyo vichafu na vya kinyama kwa kificho, kwa watoto wadogo 🐒
 
Back
Top Bottom