Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo aagiza kushushwa vyeo kwa walimu wakuu ambao shule zao zilifanya vibaya

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma, Chande Nalicho ameagiza kushushwa vyeo wakuu wa shule zote za msingi na sekondari katika wilaya hiyo, ambao shule zao zimefanya vibaya katika matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi na sekondari mwaka 2015/2016.

Aidha amewataka wenyeviti na wajumbe wa bodi za shule kujipima uhalali wao kama wana sifa ya kuendelea kuwemo katika nyadhifa zao, kutokana na matokeo mabaya yaliyopata shule wanazozisimamia ambayo yameitia aibu wilaya hiyo.

Alisema wenyeviti na wajumbe wa bodi ni lazima waachie ngazi kwani shule zao zimefanya vibaya na imeonekana sababu mojawapo ya kufanya vibaya kwa shule hizo ni walimu kutowajibika.

Alisema wameshindwa kuwafuatilia na kushindwa kushirikiana na wazazi kutatua changamoto mbalimbali zinazozikabili shule zao.

Nalicho alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na wakuu wa shule nne za sekondari, wajumbe na wenyeviti wa bodi za shule hizo zilizofanya vibaya katika matokeo ya kumaliza elimu ya sekondari mwaka uliopita.

Alikutana nao katika kikao maalumu cha kazi na baadhi ya watumishi wa kata ya Lusewa kilicholenga kutafuta majawabu juu ya kero zinazowakabili wakazi wa kata hiyo.

Shule zilizofanya vibaya katika matokeo hayo ni Lusewa, Msisima, Kwizombe na Matepwende.

Aliwataka walimu na wakuu wa shule hizo kuongeza juhudi katika kuwasaidia watoto madarasani ili waweze kufanya vizuri katika masomo yao.

“Sitakubali mwaka ujao kuona shule zenu zinaendelea kushika mkia, ninyi ndiyo chanzo cha wilaya yetu kushika nafasi ya pili kutoka mwisho katika matokeo ya mitihani ya mwaka jana. Nataka muongeze juhudi katika kazi zenu, tumieni muda mwingi kuwafundisha hawa watoto madarasani, badala ya kutumia muda wenu kwa ajili ya kufanya anasa,” alisema Nalicho.

Alisema suala la elimu ni muhimu katika maisha ya binadamu kwani hakuna anayeweza kufanikiwa katika maisha yake kama hajakwenda shule.

Aliwasisitiza kuwa muda umefika kwa wakazi wa kata hiyo kuona aibu na matokeo hayo, badala yake wahimize watoto wao kupenda shule kwa kuwa elimu ndiyo urithi bora kwa mtoto.
 
Huyo mkuu wa wilaya mwalimu wangu amenifundisha iyunga boys mbeya 1 mchapa kazi sana ponge la teacher huyo japo now mkuu wa wilaya safii
 
Bila kutatua changamoto zinazozikabili hizo shule hayo matamko hayana maana.
 
Kazi ya kufaulisha wanafunzi si ya mwalimu,ni jitihada ya mwanafunzi,mwalimu anaweza kufundisha na matokeo yake ndiyo hayo
 
Hivi hawa wakuu wa wilaya na mikoa wanajua na majukumu yao ya kazi kweli? Kama shule zimeshindwa na ziko wilayani kwake kwanini asimuhoji mkurugezi na mkurugenzi amuhoji afisa elimu tatizo nini? Leo anakurupuka kuwaadhibu walimu wakati kuna matatizo mengi mashuleni likiwepo la mishahara na marupurupu ya walim halafu Ati anadai mwakani hataki kuona upuuzi huo anauhakika gani kwamba atateuliwa tena na kubaki ktk wilaya hiyo? Si kila wakati ni wa siasa
 
Huyo mkuu wa wilaya hana weledi wa kutosha kuhusu anachozungumzia. Mtiriko wa kiutendaji ulihitaji yeye azungumze na Mkurgenzi mtendaji wa halmashauri hiyo pamoja na Afisaelimu wilaya kuliko yeye kuwaruka na kukutana na walimu moja kwa moja labda kama katika kikao hicho maafisa niliowataja walikuwapo hapo itakuwa sawa, vinginevyo anawaonea walimu tu.
Pia afahamu kuwa Mtu hawezi kuvuna asipopanda, hivyo anatakiwa kufahamu kuwa kufaulisha wanafunzi katika mitihani kunataka uwekezaji mkubwa, sasa ofisi yake imewekeza kiasi gani katika elimu wilayani humo? Nahisi naye ni Jipu tu ila anataka kujionesha tofauti.
 
Mazingira nayo huchangia wanafunzi kufaulu,anaona nini cha kumvutia asome kwa bidii afikie malengo
 
HUU UNAANZA KUWA UNYANYASAJI.WALIMU WALIKUWA WANAPELEKEWA WATOTO WASIOJUA KUSOMA,INTAKE ZAO BADO.HAZIJAISHA MASHULENI.KWA SKONDARI WANGETOA MIAKA MITATU YA KUTEKEBISHA HALI HIYO NA SII KUWASHUSHA VYEO.HUYO WANAEMUEKA WATAMSHUSHA TUU KWA HALI ILIVOKAA.HII NI ZAIDI YA KUKURUPUKA.NA IVI VYEO VITAUMIZA WENGI SANA.
 
vita vya walimu vina hali kama ya unyanyasaji.watu wanapewa watoto mia mbili darasani.hujarekebisha chochote unaanza kumfukuza huyo mwalimu.navojua mwalimu ana asilimia 50 Kielimu kwa mtoto na mzazi 50.siyo na sisi wazazi tutakuja kuitwa mashuleni na.kuchapwa viboko .shikamoo hapa kazi tu.
 
  • Huyu jamaa naona anatembelea nyota ya JPM, Infact hata hizo shule anazoongelea hazina maabala wala walimu wa kutosha..
  • Kazi ipo kwa kweli Mwaka huu..
 
Back
Top Bottom