Mkuu wa Wilaya ya Magu mkoani Mwanza, Salum Kali amewaagiza viongozi wa vitongoji na vijijini wilayani humo kuwashughulikia mafataki wote

Nyanswe Nsame

Senior Member
Jul 9, 2019
158
175
DC Magu - "tutawakamata wazazi, walezi na mafataki wote"

Mkuu wa Wilaya ya Magu mkoani Mwanza, Salum Kali amewaagiza viongozi wa vitongoji na vijijini wilayani humo kuwashughulikia watu wanaokatisha wanafunzi masomo kwa kuwapa ujauzito.

Mkuu huyo wa wilaya amesema, pamoja na kuwashughulikia "mafataki" hao pia wanapaswa kuwakamata wazazi na walezi ambao watoto wao wanapewa ujauzito lakini wanaficha wahalifu.

Kali ametoa agizo hilo jana wakati alipozungumza na baadhi ya viongozi wa ngazi ya vitongoji na vijiji kutoka kata mbili za Ndagalu na Itumbili wilayani humo.

Amesema baadhi ya wazazi na walezi ambao watoto wao wanapewa ujauzito lakini wao wanawaficha watuhumiwa kwa kurubuniwa na fedha na wao wanapaswa kushughulikiwa kama wahalifu.

Kali amesema katika wilaya hiyo, atahakikisha wazazi wote wanaoshirikiana na watuhumiwa wanaowapa ujauzito wanafunzi chini ya miaka 18 wanatiwa mbaroni ili kutokomeza tatizo hilo.

"Kuna baadhi ya wazazi unakuta watoto wao wanapewa ujauzito, lakini mzazi kwa tamaa zake anarubuniwa kwa kupewa pesa kidogo anamwambia mwanae amfiche aliyempa ujauzito.

"Hiyo tabia katika wilaya yetu ya Magu nataka ikome, nitawashughulikia wale wote wanaofanya vitendo hivyo ikiwemo kuwafikisha kwenye vyombo vya dola maana tukiacha hii tabia itakatisha ndoto za watoto wengi.

"Watoto hawa baada ya kuambiwa na wazazi wao wawafiche waliowapa mimba kwa ahadi ya kulelewa na huyo aliyempa mimba kweli na wao wanaficha.

"Tamaa hizo za siku chache wanaamua kuachana na elimu ambayo ingewasaidia katika maisha yao ya baadae na wazazi wao," amesema Kali.

Katika nyingine mkuu huyo wa wilaya amezungumzia sheria ya siku 90 ya mwanafunzi kufutwa shuleni baada ya kukosekana kwa siku hizo kwa kudai wilaya hiyo haitafanya hivyo.

Amesema kwenye wilaya hiyo, watakuwa wanaendesha msako wa kuwatafuta wanafunzi watoro ambao wamekimbia masomo na kurejeshwa shuleni kuendelea na masomo.

"Hata kama mwanafunzi atakaa siku 90 hayupo shuleni tutamtafuta na kumleta aendelee na masomo lakini pia tutamtafuta yule aliyesababisha utoro ashughulikiwe.

Kali amesema wilaya hiyo inafanya hivyo, kutokana na elimu nchini kutolewa bure bila malipo yoyote yale.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo kiserikali la kutetea haki za Wanawake na Wasichana la Kivulini jijini Mwanza, Yassin Ally amesema janga la wanafunzi kupewa mimba nchini limekuwa halipewi kipaumbele.

Amesema ni jambo la kushangaza kuona tatizo la kutokomeza au kuondoa mifupo ya plastiki mtaani likifanyika kwa kasi kubwa lakini tatizo la wanafunzi kupewa ujauzito kutokupewa nafasi.

"Kasi ya kuondoa mifuko ilifanyika kwa haraka sana nchi nzima inakuaje tunashindwa kuhamishia kasi hii katika kuondoa mimba za utotoni," amesema Yassin.

Alisema suala la kupambana na mimba za utotoni lipo kwenye mpango wa Taifa wa miaka mitano ya Serikali ya kutokomeza ukatili wa wanawake na wasichana hivyo akahimiza jamii kuwa mabalozi kutokomeza mimba za utotoni.

Yassin alitolea mfano kuwa, viongozi wa vijiji na kata wamekuwa wakishirikiana kutafuta mbuzi aliyepotea kwa wiki mbili lakini anashangaa kuona nguvu hiyo ikishindwa kutumika kutokomeza mimba za utotoni kwenye maeneo yao.
 
Elimu inamsaidia nani bwana tusilazimishane. Unashawishi vipi watoto wasome wakati wanaona maelfu ya graduates mitaani hawana dira na yeye anaona fursa na hataki kupoteza muda?
 
Back
Top Bottom