Mkuu wa Wilaya ya Ileje Mheshimiwa Rosemary, amemuweka ndani mkurugenzi wa Wilaya yake

nyanile

Senior Member
Jan 8, 2015
102
30
Hatimaye yale Mabadiliko ya Kweli na kuacha kutenda kwa Mazoea ndani ya Ofisi za umma aliyokuwa akiyazungumza sasa yamezidi kuendelea kufanya kwa vitendo.

Mkuu wa Wilaya ya Ileje mkoani Songwe mh Rosemary Senyamule,alitumia mamlaka yake ya katiba kumweka ndani (lock up) Mkurugenzi wa Wilaya ya Ileje ndugu Kwembe, kwa sababu ya kupuuza agizo lake la kutengeneza X ray machine ya hospitali ya wilaya ambayo imekuwa kero sana kwa wananchi wa wilaya ya Ileje.

Mh mkuu wa wilaya alifikia hatua hasa baada ya kumkabidhi za milioni13 alizochangisha kwa harambee kutoka kwa wadau mbalimbali wa Maendeleo ili kuhakikisha machine hiyo inatengenezwa mapema zaidi. Mbali na kutokutengeneza hiyo machine, mkurugenzi huyo pia katika ziara mkuu wa Mkoa ya 15/06/2016 alibadilisha ratiba hiyo bila mkuu wa wilaya huyo kushirikishwa na kupelekea mkuu wa Mkoa mh Chiku Ghalawa kukosa fursa ya kuikagua miradi mbalimbali ya Maendeleo na kuleta hisia ya uwezezekano wa kutofanyika kwa miradi hiyo au kufanywa chini viwango.

#Hapa Kazi Tu, Tuendelee Kumuunga Mkono Rais Magufuli
 
Kwa nchi hii, huyo aliyewekwa ndani ndio atakuwa mshindi mahakamani ikitokea anashitakiwa.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kama mkurugenzi huyo amekula hiyo 13M, bila shaka DC anaweza kumshitaki polisi na polisi wakamkamata na kumweka ndani wakisubiri kukusanya ushahidi ili wamshitaki.

Kama hatua hii imepitiwa, basi hakuna tatizo huyo bwana Kwebe anaweza kulala huko ndani hadi Jumatatu.

Mleta mada hujapanga vizuri hii habari, ifanyie marekebisho.
 
Dalili mbaya, kwamba mtu anafurahia kwa sababu kiongozi kawekwa ndani na kudai haya ndiyo maendeleo! Ukiisoma taarifa hiyo inaonyesha tatizo la kiuongozi, mkuu wa Wilaya anafikiria maslahi yake na zaidi kuliko ufanisi wa kiuongozi wa wilaya.
 
wajibika au utakwenda gerezani - hakuna kula mshahara wa bure ambao ni jasho la wananchi
 
Pamoja na nia yake njema ya kutaka uwajibikaji na kutii mamlaka lakini kwanza angetafuta msaada wa kisheria hasa kwenye kipengele cha kumuweka lock up mtumishi wa umma cheo cha ukurugenzi, taratibu za kuwajibishana na uhusika wa mwajiri linapotokea tatizo
Nasema hivyo kutokana na uzoefu wa nyuma ambapo serikali kwa maamuzi ya kukurupuka iliishia kushindwa mahakamani na kuishia kulipa fidia mamilioni kwa mabilioni
......pamoja na nia njema sana lakini ni vema kufuata kanuni taratibu na sheria za njia kwa mujibu wa katiba
 
Bado sijaona mantiki ya kumuweka ndani,ama sjaelewa vizuri. Kawekwa ndani kwa kosa la kuuchelewa kufanya matengenzo ya mashine ya x- ray! , ngoja nifuatilie vizur hili suala kungine,au kuna sababu nyingine chini ya kapeti?
 
Back
Top Bottom