Mkuu wa Wilaya ya Geita katka kashfa nzito

nkomelo

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
216
44
Mkuu wa wilaya ya Geita Bwn Sherutete, ameingia kwenye kashifa mbaya ya matumizi mabaya ya madaraka yake. Hayo yamebainika katika kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo baada ya kubaini msaada unaotolewa na Geita Gold Mine kwaajili ya kusomesha watoto waliokatika mazingira magumu umechakachuliwa na mkuu huyo wa wilaya kwa kumwingiza anaedaiwa kuwa mwanae aitwae Robert Sherutete.

Kutokana na hali hiyo madiwani katika kikao chao hicho waliweka azimio la kumkataa bwana DC kwakuwa amekika maadili ya uongozi na kwamba msaada huo haukulenga watoto wa viongozi kama Dc. Madiwani hao wamesema huenda ndiyo maana uongozi wa GGM unakiburi sana mbele ya uongozi wa Halmashauri maana mkuu wa wilaya anasomeshewa mwanae na mgodi huo.
Nawasilisha.
SOURCE: Geita full council 13th July,2011
 
Yataisha hayo...! DC ni mtu mkubwa na ana watu wazito nyuma yake! Wataweza hao madiwani masikini wenzangu wachumia tumbo..!!? Naona hapo ni kama kupima lori ktk mzani wa dukani kwa Masawe. Kumbuka DC anawajibishwa na mamlaka iliyomteua.... Magogoniiiii.. Daslama. Poleni madiwani bai ze wei!
 
Hii mada si iko hapa leo siku kadhaa was it necessary to have a new topic on the same thing ? Jamani au mie ndiye nakosea juu ya jambo hili ?
 
Madiwani wanapaswa kutumia Busara na akili katika maamuzi yao lasivyo wanamwonea DC, mimi namuunga DC Mkono yupo sawa. Lasivyo Madiwani wanapaswa kuoyesha kwa ushahidi thabiti kabisa kuwa mtoto wa DC hayupo kwenye mazingira magumu!

Yes yupo kwenye mazingira magumu, na ndio maana ameweza kusoma katika hali hiyo lasivyo angekuwa na watoto wa wakubwa wenzake Ulaya na kwenye zile shule zinazoitwa International schools za karo Tsh.10.0milion kwa mwezi ijue kwa mwaka! Madiwani it's upon you to prove this.
 
Sidhani kama ni mtoto wake, huenda akawa mtoto wa ndugu yake ambaye hana uwezo. Lakini kama ikidhibitishwa kuwa ni mtoto wake wa kumzaa basi hapo kuna kitu inabidi aeleze na kama maelezo hayatatosha basi wafanye audit vizuri ya watoto wote wanaosomeshwa kujiridhisha kuwa kweli wanastahili. Nadhani kama ni tabia yake basi atakuwa ameshafanya mara nyingi tu kwa watoto hata wa marafiki zake hivyo watamkamata tu.
 
Kuna haja ya uchunguzi wa kina kufanyika na kama akibainika awajibike na maauzi magumu yafanywe dhidi yake.Hii wilaya ina mdudu nakumbuka pia Halima Mamuya aliyekuja kuwa Katibu Mkuu wa UWT aliharibu sana akiwa Geita kwa kupewa mlungula na kukumbatia tenda zote za mgodi huo huo wakati ukuwa under construction.Mama huyu aliondolewa Geita na kupewa mamlaka makubwa zaidi ya Ukatibu mkuu UWT.Haya ndo magamba asilia.
 
Huwezi jua labda mwanae anaishi katika mazingira magumu,yataisha tu bado kitambo kidogo tu.
 
Back
Top Bottom