Mkuu wa Wilaya Serengeti aliyeteuliwa kimakosa aaibishwa kwa kutolewa nje ya Ukumbi Ikulu

sohwa

JF-Expert Member
Dec 28, 2015
1,039
772
UTEUZI: Leo, Nurdin Babu ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Serengeti kuchukua nafasi ya Emile Ntakamulega ambaye alitajwa kimakosa.

==============

Nlikuwa natizama hapa Azam two (Kama sijakosea) ghafla mkuu mmoja wa wilaya Mteule akaambiwa atoke nje/atupishe kwani aliteuliwa kimakosa bila hata ya kuambiwa neno kama samahani au ishara yoyote ya kuonesha kuwa wamemletea usumbufu,lakini kuambiwa'tupishe'kwani uliteuliwa kimakosa!!!

Mimi naona ingefaa Sana kama angefuatwa alipoketi aambiwe bila hata ya watu wengi kunotice kuwa hakustahili kuwapo pale(kwamba kuteuliwa kimakosa na aombwe radhi kwa usumbufu), Lakini Haikuwa Hivyo, badala yake Katolewa nje wazi wazi.

Mnalionaje hili Wakuu?

 
Serikali ya mizukaaaa


#sugu.rais.wa. mbeya
 
Ndiyo maana mnaitwa malofa!! Ni nani huyo ameteuliwa kimakosa!! Serikali ya kukurupuka hii!!!

"Nlikuwa natizama hapa azam two,(Kama cjakosea) ghafla mkuu mmoja WA wilaya Mteule akaambiwa atoke nje/atupishe Kwani aliteuliwa kimakosa,,bila hata ya kuambiwa neno Kama samahani au ishara yoyote ya kuonesha kuwa wamemletea usumbufu,lakini kuambiwa'tupishe'kwani uliteuliwA kimakosa!!!
Mimi naona ingefaa Sana kama angefuatwa alipoketi aambiwe bila hata ya watu wengi kunotice kuwa hakustahili kuwapo pale(kwamba kuteuliwa kimakosa na aombwe radhi kwa usumbufu),, Lakini Haikuwa Hivyo, badala yake Katolewa nje wazi wazi,, mnalionaje hili Wakuu???"

Jee hiyo hapo juu ni uungwana?
 
Sanaa katika ubora wake, kama alimteua kimakosa kwanini hasingetangaza siku hile hile kubatilisha taarifa au msigwa anakazi gani.....?? Sema labda alikua na kisasi nae akaona aje amuaibishe mbele ya kadamnasi tu maana jamaa nae mtu wa visasi hatari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…