Mkuu wa Wilaya Serengeti aliyeteuliwa kimakosa aaibishwa kwa kutolewa nje ya Ukumbi Ikulu

Hapo hapo anakwambia nimewachunguza nawajua mpaka na majina na tabia zao mmoja mmoja.
Anyway back to business kama ni kweli kwamba walimwambia jamaa "tupishe" walitumia lugha isiyo nzuri kabisaaaa. Huo ndio ukweli, angefatwa aambiwe taratibu tena pasipo wakulia wala kushoto kujua ukweli wowote maana hakujipeleka ni makosa yao.
 
Okey mkuu, kama ndiye,!Nafikiri Kama kuna watu Walikuwa wanaangalia watatuambiwa Ni nani kwa jina.
Mbona utenguzi wake ulikuwa siku ile ile nadhani ni wa igunga, kiherehere Chake tu mbona taarifa ya kutenguliwa ilitoka mapema au hana tv/radio au account Facebook?
 
"Nlikuwa natizama hapa azam two,(Kama cjakosea) ghafla mkuu mmoja WA wilaya Mteule akaambiwa atoke nje/atupishe Kwani aliteuliwa kimakosa,,bila hata ya kuambiwa neno Kama samahani au ishara yoyote ya kuonesha kuwa wamemletea usumbufu,lakini kuambiwa'tupishe'kwani uliteuliwA kimakosa!!!
Mimi naona ingefaa Sana kama angefuatwa alipoketi aambiwe bila hata ya watu wengi kunotice kuwa hakustahili kuwapo pale(kwamba kuteuliwa kimakosa na aombwe radhi kwa usumbufu),, Lakini Haikuwa Hivyo, badala yake Katolewa nje wazi wazi,, mnalionaje hili Wakuu???"

Jee hiyo hapo juu ni uungwana?
Angetakiwa kuombwa msamaha jamani hiyo kitu inauma sana kweli kuaibishwa mbele ya kadamnasi bila hata aibu.nimesikitika sana jinsi watu wanavyojisahau wakipata vinafasi .Very unprofessional
 
Unajua serikali inapotaka kufanya kazi kwa kujitofautisha na awamu nyingine ni taabu kweli. Siyo kumtaka radhi yaani anapaswa kulipwa kwa sababu zifuatazo:-
1. Wamemsumbua kisaikolojia maana alijiandaa kuwa mkuu wa wilaya lakini kumbe sivyo
2. Muda wa kufika pale unapaswa kulipwa
3. Usumbufu
4. Kudhalilishwa
 
''Kuna mabadiliko madogo tuliyoyafanya kutokana na jina lilikosewa, kwa hiyo aliyestahili tumeshamuweka.''

Nadhani atakuwa huyu
 
Back
Top Bottom