Mkuu wa Wilaya Serengeti aliyeteuliwa kimakosa aaibishwa kwa kutolewa nje ya Ukumbi Ikulu

niliona jana hii habari kama sio fb basi ni humu humu jf, kuwa mkuu wa wilaya hewa, kwani watu wanatafuta faili lake hawajawahi kumsikia hata kupata tetesi, wakasema inawezekana ni mkuu wa wilaya hewa, kumbe kaibuka, maskini sielewi atajifikiriaje, atakuwa na msongo mkali sana
 
Nlikuwa natizama hapa Azam two (Kama sijakosea) ghafla mkuu mmoja wa wilaya Mteule akaambiwa atoke nje/atupishe kwani aliteuliwa kimakosa bila hata ya kuambiwa neno kama samahani au ishara yoyote ya kuonesha kuwa wamemletea usumbufu,lakini kuambiwa'tupishe'kwani uliteuliwa kimakosa!!!

Mimi naona ingefaa Sana kama angefuatwa alipoketi aambiwe bila hata ya watu wengi kunotice kuwa hakustahili kuwapo pale(kwamba kuteuliwa kimakosa na aombwe radhi kwa usumbufu), Lakini Haikuwa Hivyo, badala yake Katolewa nje wazi wazi.

Mnalionaje hili Wakuu?
UKURUPUKAJI at the highest stage.
Nani asiyeijua hii serikali ya ukurupukaji.?
 
Kumbe Rais anashauriwa vibaya hivi, sasa ya nini kumteua alafu baadae anaonekana sio mlengwa au hatofaa ktk wadhifa husika, kuna sarakasi fulani hapo
 
Kweli si ustaarabu sema uzuri jamaa mwenyewe aliyefanyiwa ni mstaarabu ningekuwa kama mimi lazima ningebwatuka mana inauma
 
na mm nilikuwa naangalia japo jina na mm nimeshidwa kulishika ila anaechukua nafasi yake anaitwa nurudini babu alikuwa rufiji ila amemwambia bahati mbaya huwa yanatokea na wamemwomba samahani nadhani wataenda kuyamaliza
 
Back
Top Bottom