Mkuu wa wilaya Iringa Kasesela akutana na wanakijiji wa Makongati waliofukuzwa na mwekezaji

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,513
kase3.jpg

index.jpeg

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe Richard Kasesela leo alikutana na wana kijiji cha Makongati ambao wamefukuzwa na mwekezaji kwenye shamba ambalo wamekuwa wanalima zaidi ya miaka 20. Wananchi karibu 281 wamekuwa wakilima shamba hilo kwa muda mrefu wakati huo likimilikiwa na mwekezaji George Emmanuel.

Baada ya kufariki Bwana George Emmanuel shamba hilo limemilikiwa na mwanae Stephen Rosy Emanuel. Baada ya kumilki mtoto wake akaamua kuwaondoa wananchi hao wengine wakiwa wamelima mazao yao, yeye akapitisha trekta na kulisha mifugo.

Ndipo wananchi kupitia kwa katibu wa CCM Iringa Vijijini Bwana Dod Sambu wakaomba wamuone Mkuu wa wilaya. Akisikiliza kero hizo Mkuu wa wilaya aliamuru mwekezaji kuacha kuwabughudhi wananchi hao.

Pia akaaamuru mwekezaji huyo ajipange kupunguza ardhi hiyo kuwagawia wananchi amabo maisha yao yametegemea hapo. Kutokana na sakata hilo ilionekana mtendaji wa kijiji amekuwa asikilizi kero za wananchi badala yake amehamia na kuishi nyumba za mwekezaji, Mkuu wa wilaya aliamuru Mkurugenzi amsimamishe kazi mara moja Mtendaji huyo na uchunguzi ufanyike haraka ikiwemo tuhuma za kuchangisha 10,200 pesa za kuandikisha cheti cha kuzaliwa kwa wananchi zaidi 100 bila kuzifikisha RITA.
⁠⁠⁠⁠
⁠⁠Wananchi walimshukuru sana Mkuu wa wilaya akizungumza mama Veronica Sanga alisema " baba Mkuu wa wilaya Mungu akubariki sana leo nitalala usingiz ambao sijalala wiki nzima baada ya mahindi yangu yoote kuliwa na ng'ombe "

Shamba namba 820 lililopo Weru na kati ya mashamba ambayo yalimilikwa toka mwaka 1820 na baadae hati yake kuiisha mwaka 1999 na baadae kuhuishwa mwaka 2006 kwa miaka 33 mingine. Shamba lenye ukubwa wa zaidi ya hekta 2000 lipo kata ya Maboga kijiji cha Makongati na mpaka sasa hati yake inasomeka mmiliki ni Bwan George Emmanuel.
 
Back
Top Bottom