Mkuu Wa Wilaya Avutana Mashati na Walinzi Wa Night Club

Katambi anapenda vurugu hats udom nadhani aliwahi timuliwa kwasababu za kuhamasisha mivurugu na maandamano nabado anamabeef na mkurugenzi Dom. Kifupi vijana wa chadema wanajua kuropoka lakini hawaujui uongozi. Tizama huyo,mtizame shonza,mfatilie kafulila na wengine kibao,wanakiherehere flani hivi...
 
Hii ajabu sana Yani mkuu wa wilaya ambaye ndiye mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya badala ya kuwa mfano wa kuigwa katika jamii yeye anakua mwanzisha vurugu? kwani hata angelipa na kuwalipia hao watu wake kulikuwa na shida gani? kingilio chenyewe elfu 10 kama disco toto tu, alafu unataka dezo? hajui kwamba watu wanafanya biashara na wanalipa kodi kwa kazi hiyo
 
Habari za Jumapili Wanajamvi.

Jana usiku jijini Dodoma kuliandaliwa onyesho la msanii wa muziki wa Bongo Fleva Nay wa Mitego kwenye Klabu ya Usiku maarufu Royal Village Au Club Seven.

Kama raia wa kawaida, niliamua na mimi nihudhurie ndipo nikajongea maeneo hayo muda wa saa saba kasoro usiku.

Kiingilio cha onyesho hilo kilikuwa ni Shilingi Elfu Kumi (10,000/=) tu. Na tickets za kuingia ndani zilikuwa zikiuzwa kwenye gari(Noah) la Royal Village pale geti la kuingia Club Seven na Ngalawa Bar.

Wakati naulizia taratibu za ununuzi wa tiketi ya kuingia kwenye onyesho hilo, ukazuka mzozo pale getini kati ya walinzi na watu ambao sikuwatambua kwa muda ule. Niliposogea karibu, nikapokelewa na tukio la dada mmoja akipigwa kofi la haja na mlinzi(bouncer) aliyejazia misuli. Kwa muonekano huyo dada alikuwa amelewa na alikuwa akizozana na walinzi huku akitaka kuingia ndani. Baadae nilikuja kufahamishwa kuwa dada na vijana wengine kama wanne hivi walikuwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mh. Patrobas Katambi.

Hali ilivyokuwa inaonekana, chanzo cha mgogoro huo ni kuwa msafara wa Mkuu wa Wilaya ulitaka kuingia ukumbini hapo bila ya kulipia kiingilio. Na pia msafara huo ulijitambulisha kibabe pale getini.

Ila tendo la yule mlinzi (bouncer) kumtia banzi yule dada, halikumfurahisha Mheshimiwa. Ndipo nae akaanza kuhamaki na kutaka kushikana na yule bouncer huku watu wakiwavuta wasipigane.

Ilifikia wakati Mheshimiwa alivua koti lake la suti na kubakia na t-shirt ya rangi ya ugoro yenye nembo kubwa ya taifa ya rangi kwa mbele. Hapa ilikuwa inamaanisha Mheshimiwa alikuwa anajiweka tayari kwa ajili ya kupambana na mlinzi aliyempiga mtu wake.

Baadae alikuja kiongozi wa eneo lile na akaamua kumuondoa yule mlinzi. Kisha akaenda kuongea na Mheshimiwa kwa muda mrefu. Nadhani alikuwa akiomba radhi kwa yaliyotokea.

Baada ya hayo yote, nikaona ni bora nisinunue tiketi ya onyesho hilo ili kukwepa hasara pale Mheshimiwa atakapochukua hatua ya kulifungia onyesho hilo kwa sababu za kiusalama. Ndio! Yeye kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, anaweza kutoa amri ya kusitishwa kwa onyesho lile kisa tu dada aliyekuja nae kapigwa na bouncer.

Pia niliamua kuondoka kabisa eneo hilo na kuhamia eneo lingine. Hivyo sikujua nyuma huko walimalizana vipi.

Ushauri wangu kwa Wanasiasa Vijana
1. Mnapoenda kwenye maeneo ya starehe epukeni kuwa na kiburi cha cheo chako. Na uangalie wale ulioambatana nao wasije kukutia doa.
Fuateni mifano ya kina Joseph Haule (MB) na Joseph Mbilinyi (MB) wawapo maeneo haya, hutaweza fahamu kirahisi kama wapo. Hawaambatani na msululu wa watu wengi.

2. Ndg. Patrobas Katambi ilikuwa atumie akili ndogo tu ya kumuita au hata kumpigia simu Meneja wa eneo lile kuwa yeye na watu wake kadhaa wanataka kuhudhuria. Sidhani kama angekataliwa.

3. Epukeni ulevi wa madaraka kwa kutisha watu kwa kauli za "UNANIJUA MIMI NI NANI". Sio kila raia atakujua kuwa wewe ni Mkuu wa Wilaya.

NIMESHUKURU KUONA LILE BANZI LA MLINZI HALIJATUA USONI MWA MHESHIMIWA!!!

Naomba kuwasilisha.
Bila clip haya ni mavi tu,tena ya nguruwe pori

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hao sio wa CDM ni mafisiem menzenu
Katambi anapenda vurugu hats udom nadhani aliwahi timuliwa kwasababu za kuhamasisha mivurugu na maandamano nabado anamabeef na mkurugenzi Dom. Kifupi vijana wa chadema wanajua kuropoka lakini hawaujui uongozi. Tizama huyo,mtizame shonza,mfatilie kafulila na wengine kibao,wanakiherehere flani hivi...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom