Mkuu wa Wilaya Acharazwa Bakora | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkuu wa Wilaya Acharazwa Bakora

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 5, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Ili asisahau ahadi alizozitoa wakati wa kampeni za uchaguzi, mkuu wa wilaya moja nchini Peru alimualika mtu amcharaze bakora mbele ya umati wa watu.
  Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 23 wa nchini Peru ambaye alichaguliwa kuwa mkuu wa wilaya alitumia njia ya aina yake ya kujikumbusha ahadi alizozitoa wakati wa kampeni wa uchaguzi.

  Abraham Carrasco baada ya kuchaguliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Chilca, aliamua kuwaita watu kushuhudia akicharazwa bakora kabla ya kula kiapo cha kuitumikia wilaya hiyo.

  Mbele ya mamia ya watu waliokusanyika, mkuu huyo wa wilaya alicharazwa bakora tatu ili azikumbuke ahadi alizozitoa wakati wa uchaguzi.

  Carrasco alimchagua mzee mmoja aliyekuwa akiheshimika katika wilaya hiyo ndio amcharaze bakora kabla ya kula kiapo.

  "Usiwe mwizi", alicharazwa bakora ya kwanza, "Usiwe muongo", alicharazwa bakora ya pili "Usiwe mvivu", alicharazwa bakora ya tatu.

  Baada ya kucharazwa bakora, Carrasco alimbusu mikono mzee aliyemchapa bakora na kisha kula kiapo cha kuitumikia vyema na kwa uadilifu wilaya hiyo.

  Carrasco alisema kuwa ataihifadhi bakora iliyotumika ili iwe kumbukumbu yake kwa ahadi alizozitoa wakati wa kampeni za uchaguzi.
  source na picha zaidi hapa NIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.
   
 2. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #2
  Jan 5, 2011
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,519
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Hii style ingekuwa mandatory hapa bongo, maisha yangekuwa bomba
   
Loading...