Mkuu wa shule ya sekondari ajinyonga, chanzo ni upweke baada ya ulevi

Benjamini Netanyahu

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
92,270
111,782
the_betrayal.jpeg
MKUU wa Shule ya Sekondari Tumuli katika Wilaya ya Mkalama, mkoani Singida, Richard Makala (58) amejinyonga kwa kamba kutokana na kile kinachodhaniwa kuelemewa na upweke.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Debora Magiligimba, amesema mjini Singida kuwa, Makala alijinyonga jana saa 1 asubuhi.

Ameeleza kuwa Makala alikutwa amejinyonga kwa kutumia kamba iliyotengenezwa kwa vipande vya chandarua iliyofungwa juu ya mti umbali wa mita 130 kutoka nyumbani kwake.

Amesema, chanzo cha tukio hilo hakijajulikana na kwamba hakuna mtu au watu wanaoshikiliwa kutokana na tukio hilo na kuongeza kuwa polisi inaendelea na upelelezi kubaini kilichomsibu mwalimu huyo.

Hata hivyo, Mjumbe wa Bodi ya shule hiyo, Mabruki Ng’ui amelisema mwalimu huyo alikuwa anaishi peke yake kwa muda mrefu baada ya mkewe ambaye ni Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Tanzania (KKKT) Kitusha wilayani Iramba kuamua kutengana naye kutokana na unywaji pombe.

"Huyu bwana amekuwa kwenye ndoa ya jina tu maana mke wake amekuwa akiishi mbali naye kwa kipindi kirefu sana, amekuwa mpweke kwa muda mrefu mno huenda hicho ndicho kilichosababisha ajitoe roho yake," amesema Mjumbe huyo wa Bodi.

Makala ni mzaliwa wa kijiji cha Ndago, wilayani Iramba na anatarajiwa kuzikwa leo nyumbani kwake.

Ameacha mjane na watoto watano.

IMEANDIKWA NA ABBY NKUNGU-HABARILEO SINGIDA

Chanzo: Malunde Blog
 
baba mchungaji maskini? alishanyimwa papuchi wee akaona isiwe taabu.halafu unakuta mke kanisani anafundisha semina za ndoa
Mwalimu wa sekondari sio mchungaji, mrs ndio mchungaji sasa alikimbia ulevi wa marehemu! Sijui siku ya msiba ataenda au atapotezea! na mafao ya marehemu atahusika kuyadaka kumbe labda yeye ndie source ya mauti ya mzee wake! Wanawake tujifunze uvumilivu katika ndoa zetu.
 
Tulieni kwenye ndoa
 
mke wa mchungaji anaitwa mama mchungaji so mume wa mchungaji atakuwa baba mchungaji upo?
 
Back
Top Bottom