John F Molel
Member
- Dec 30, 2017
- 6
- 0
Mkuu wa Mkoa wa Tabora ahimiza wananchi kushiriki zoezi la Vitambulisho vya Taifa
Akiwa katika ziara Wilayani Urambo Mkuu wa Mkoa Mh. Agrey Mwandri ametumia fursa hiyo kuwahimiza wananchi wa kijiji cha Ussoke Mlimani kujitokeza kwa wingi kusajiliwa katika zoezi la Usajili wa Vitambulisho Vya Taifa linaloendelea Mkoani humo. Pia amesisitiza wananchi kuwafichua wale wote ambao wanaishi nchini kinyume na taratibu ili waweze kugundulika kwani wananchi ndio wanaokaa nao katika jamii hivyo waisaidie serikali. Nae Mkuu wa Wilaya ya Urambo Mh. Anjelina George Kwingwa amesema zoezi la NIDA halina lengo la kuwabagua wananchi isipokuwa kila mtu atapata kitambulisho kulingana na hadhi yake (Raia, Mgeni mkaazi au Mkimbizi). Pia amewataka Viongozi wote wa kata na vijiji kutoa ushirikiano mara zoezi linapofika kwenye maeneo yao.
Mkuu wa mkoa wa Tabora Mh. Agrey Mwandri akiongea na wananchi wa kijiji cha Ussoke Mlimani na kuwahamasisha kushiriki zoezi la usajili wa Vitambulisho vya Taifa. kushoto ni Maafisa wa NIDA Emiliana Temu na Grace Msacky
Mwenyekiti wa Mtaa wa Ussoke Mlimani Bw. Jackson Kitwe (kushoto/mwenye kofia) akiwaahidi Mkuu wa Mkoa Mh. Agrey Mwandri na Mkuu wa Wilaya ya Urambo Mh. Anjelina George Kwingwa kutoa ushirikiano ili kufanikisha zoezi la usajili
Afisa Usajili mkoa wa Tabora Bi Grace Msacky akiwa na Mkuu wa Mkoa Mh. Agrey Mwandri wakati akiwahamasisha wananchi kujitokeza kusajiliwa na mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa usajili
Wananchi wa Kata ya Mpella wakiwa wamekusanyika kwenye ofisi ya Kata ili kuhojiwa na Maafisa Uhamiaji ili kukamilisha hatua za mwanzo za usajili