Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Zerothe Stephen aagiza wakuu wa shule zinazofanya vibaya kukiona cha moto

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Habari wanaJF,

Katika juhudi za kukuza na kuimarisha sekta ya Elimu katika ngazi ya mkoa basi Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Zelothe Stephen aagiza wakuu wa shule zinazofanya vibaya mkoani humo wachukuliwe hatua za kinidhamu.

Ikumbukwe mkuu wa mkoa huyu pia aliwahi kumuagiza Kamanda wa Polisi mkoa huo, Jacob Mwaruanda kuwasaka na kuwakamata watumishi hewa 18 waliobainika katika uhakiki uliofanyika katika halmashauri zote mkoani humo.
 
Ndio maana sikuwahi kuipenda hii kazi tangu nilipoanza kujitambua. Mwalimu kadharaulika sana na amekuwa mhanga wa kila mtafuta kick za kisiasa. Mara wacharazwe, mara wapokee kichapo toka kwa wanafunzi, walazimishwe kwenda kwenye maandano ya matukio ya kisiasa (kama wanafunzi wao) nk. despite of umuhimu wao.
 
Ipy ungeweka heading vema "agizo la kukiona" anyway sorry kama wazo langu lina ukakasi
 
Haangalii sababu za kufanya vibaya anatoa tu amri. Hii sekta ina changamoto nyingi.
 
SASA Mwalimu ndiye anayefaulisha mwanafunzi?.Zipo sababu nyingi zinazomafanya wanafeli mitihani.
 
Walimu wenyewe hawana umoja na msimamo ndiyo maana wanaonewa sana ingawa wapo wengi
 
Mkuu wa mkoa wa Iringa amfukuza Kazi Mkurugenzi wa manispaa Kwa kumdanganya MKUU wa mkoa kuwa hakuna mfanyakazi hewa, mbona Mkuu wa mkoa wa Rukwa nae alidanganywa Na Ras wake lakini kashindwa kumchukulia hatua?
 
Habari wanaJF,

Katika juhudi za kukuza na kuimarisha sekta ya Elimu katika ngazi ya mkoa basi Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Zelothe Stephen aagiza wakuu wa shule zinazofanya vibaya mkoani humo wachukuliwe hatua za kinidhamu.

Ikumbukwe mkuu wa mkoa huyu pia aliwahi kumuagiza Kamanda wa Polisi mkoa huo, Jacob Mwaruanda kuwasaka na kuwakamata watumishi hewa 18 waliobainika katika uhakiki uliofanyika katika halmashauri zote mkoani humo.
Mkuu wangu analo halafu na anavyojenga visasi kwa walimu unapochangia hoja ya kujenga atumbuliwe tu
 
Kwanza awaonye baadhi ya wazazi wanaowapa watoto wao pombe na viroba kabla ya kuingia darasani!
 
hahahahaha huyu naye anakuja kwa kukurupuka atakutana na waalimu wenye akili kumzidi ambao wanaandaa ushahidi khs wanafunzi hao! afu anataka wabebwe km shule za msingi :)o_O:p
 
Huyu naye naona ana mhemko.
Kakosa kazi ya kufanya, hili ndilo la kwanza kaona aoshee sura kidogo kwenye vyombo vya habari.
Hehehe, aliyechagua hawa wakuu wa mkoa na wilaya inabidi achukuliwe hatua za kinidhamu, wanaongea nonsense kila kukicha.
 
kuna shule walimu hawana viti vya kukalia achilia mbali wanafunzi halfu useme wafaulishe ni kuwaonea tu
 
Nahis sisi tunaochangia kuponda agizo la RC ndio Nonsence.
Mkuu unakosea na utaniwia radhi uelewe kua mwalimu ni sehemu tu ya mwanafunzi kufaulu ila kuna mambo mengi yanayopelekea mwanafunzi afanye vizur kwa hyo kushabikia eti waalimu wachukuliwe hatua ni kuonyesha kutokua na uelewa wa process nzima ya learning tuwe tunakuja na hoja za msingi waungwana naomba kuwasilisha
 
Back
Top Bottom