Mkuu wa Mkoa wa Dodoma afuta posho za vikao

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma afuta posho za vikao

bajeti inayokadiriwa pale bungeni haijawahi kutosha kutokana na upungufu wa pesa. kwa hiyo hiyo hela ikajazie sehemu zingine.

WanaJF, Salaam!

Nilikuwa natazama chanzo kimoja cha televisheni mchana saa nane 18/12/2015 katika habari hiyo nimemsikia akitamka kwamba kuanzia sasa hataki kuona wala kusikia habari za ulipaji wa posho za vikao kwa watumishi.

Habari hii imenishtua kidogo kwa kuwa kimsingi fedha zinazotekeleza shughuli hizo zilishaidhinishwa na kuzitumia kwa kazi nyingine bila kibali cha Wizara ya Fedha kinatoa nafasi kwa CAG kutoridhishwa matumizi ya fedha hizo.

Aidha, binafsi nadhani kilichotakiwa kufanyika ni kuanza na maandalizi ya bajeti hii kwa Makatibu Wakuu wa Wizara kuainisha maeneo ambayo katika bajeti ijayo si lazima kuzingatiwa ili fedha zake zipelekwe kwenye miradi ya maendeleo au kwingineko panapostahili.

Najiuliza maswali mengi nikitilia mashaka ya baadhi ya viongozi kutomwelewa vizuri Mhe. JPM na kuanzisha vitu vitakavyoleta chuki miongoni mwa jamii hasa itakapotokea wana habari kuripoti juu ya matumizi yasiyo sahihi ya fedha za serikali kutokana na kubadilishiwa matumizi.

Tusikurupuke, tujuwe nn tunapaswa kukifanya na matokeo yake baadae

Ushauri tu!
 
hebu nijulisheni: je, madiwani wanalipwa mishahara au vipi. na wanapotoka kwenye kata zao kwenda makao makuu ya wilaya kuhudhuria vikao (na kusema kweli kazi kubwa wanazofanya ni vikao) gharama za safari n.k. zinalipwa na nani au wanajitolea. swali la ziada: mkuu wa mkoa katika safari hiyo analipwa au vipi, na dreva wake je?
 
Hawa wakuu wa( w) na mkoa wanajipendekeza saana.saa zingine wanakwenda kwenye kazi za wakandarasi wanafoka kweli wakati hela ya kuwalipa haipo mpaka mwakani ndo hela watalipa tatizo asilimia kubwa hawa ma contractor wa bongo hajui shelia hawadai hata intrest hela mwaka mzima unasubili
 
Back
Top Bottom