Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, kupanda kizimbani

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
752
1,810
RC wa Arusha Mrisho Gambo, February 3 mwaka huu atapanda kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi Arusha, kuthibitisha ujumbe wa simu aliodai kukashifiwa, unaosema karibu Arusha tutakudhibiti kama uarabuni walivyodhibiti Mashoga.

Ujumbe huo unadaiwa kutumwa na mbunge Godbless lema na Mkewe Neema Lema ambao ni washitakiwa katika kesi ya uchochezi kwa njia ya mtandaao.

Lema na mkewe leo wamesomewa maelezo ya awali na upande wa jamhuri walidai kuwa na mashahidi watano akiwemo RC na vielelezo viwili, shauri hilo linasikilizwa na hakimu John Baro wa mahakama hiyo.

b83ceb6d3660942eafe653f72e21eeeb.jpg
 
Sasa kosa hapo ni lipi ? Ni uongo Uarabuni hawajawadhibiti mashoga ?

Mtajua wenyewe Chadema mmezidi kulia lia tu hamna hatua yoyote mnayochukua zaidi kulaani
Uko sawa mkuu, Viongozi wa CHADEMA wamezubaa Sana, wangekinukisha kabisa, Nashangaa Kwa nini walivunja ukuta hiyo ndo ilikuwa operation pekee ya kuifanya nchi isikalike hadi Dikteta uchwara angesalimu amri, angeua wangapi? angekamata wangapi? angepoteza wangapi?
Nguvu ya umma haijawahi kushindwa popote pale duniani.
 
Sasa kosa hapo ni lipi ? Ni uongo Uarabuni hawajawadhibiti mashoga ?

Mtajua wenyewe Chadema mmezidi kulia lia tu hamna hatua yoyote mnayochukua zaidi kulaani
Wewe ndo huna akili kwa hiyo unata kuwaambia viongozi watangaze kwamba jirani yako akikupiga na wewe mpige au mvizie umpige? Huoni kama itakuwa hatari watanzania bado hatuja fikia hapo acha uchochezi
 
Hayo CHADEMA wanajitakia wamekuwa waoga mno. Nadhani Mbowe na Lowasa wanafikiria usalama wa mali zao na biashara zao pia. Chama akabidhiwe Lissu hapo ni acha maneno weka muziki wa Lissu
Huyu jamaa ipo siku kila mmoja atamwelewa..
 
Uko sawa mkuu, Viongozi wa CHADEMA wamezubaa Sana, wangekinukisha kabisa, Nashangaa Kwa nini walivunja ukuta hiyo ndo ilikuwa operation pekee ya kuifanya nchi isikalike hadi Dikteta uchwara angesalimu amri, angeua wangapi? angekamata wangapi? angepoteza wangapi?
Nguvu ya umma haijawahi kushindwa popote pale duniani.
Kweli uko tayari kufa kwaajili ya chama kinachotetea ufisadi?

Ama kweli ukistaajabu ya musa...
 
Wewe ndo huna akili kwa hiyo unata kuwaambia viongozi watangaze kwamba jirani yako akikupiga na wewe mpige au mvizie umpige? Huoni kama itakuwa hatari watanzania bado hatuja fikia hapo acha uchochezi
Wewe mwenye akili ndio upeo wako ulipofikia ? Aliyekuambia hatua pekee ya kuchukua ni hiyo uliyoitaja ni nani ?
 
Ipo siku tu
Unaota ndoto,hadi unakufa hiyo siku haitotokea kamwe,watu wenyewe kama wewe hadi JF unatumia ID fake,avatar fake.unasema ipo siku? Hata viongozi wetu wakiamua kinuke hawatapata supporters maana ni waoga sana
 
kwa Kesi hii naona kama mtu akala Mvua za kutosha mwaka huu. Let's wait and see what will be happen to them.
 
Lema alijisahau san.Ujumbe kama huo ni wa nini,mtu mzima na mkeo mnakaa mnaandika uharo kama huo.Hao ni wa kufunga tu
Wewe kwa akili yako timamu unaweza kukiria kwamba ujumbe wa simu uandikwe na watu wawili? Simu hiyo na ujumbe huo una ukubwa gani wa kuandikwa na watu wawili. Kwamba mmoja aliandika akachoka ama mmoja ana dictate kwa mwenzake? Simu imesajiliwa kwa jina gani?
 
Back
Top Bottom