siyoi koroi
Senior Member
- Sep 6, 2016
- 177
- 214
Lilikuwa ni tukio la kusikitisha pale mkuu wa mkoa wa Arusha alipoenda kwenye kata ya ngarenanyuki kwa ajili ya ufunguzi wa kampeni za udiwani akiwa ameambatana na wakuu wote wa wilaya za mkoa wa Arusha pamoja na kamati zote za ulinzi na usalama za mkoa na wilaya zote za mkoa wa Arusha. Pamoja na viongozi wote wa ccm wakiongizwa na mwenyekiti wa ccm mkoa wa Arusha.
CCM Walipanga kufungulia kampeni kwenye kitongoji cha mwakey tukio ambalo lingeambatana na kitendo cha mkuu wa mkoa kwenda kuweka shada la mauwa kwenye kaburi la marehemu Diwani aliyefariki mapema mwaka jana.
Baada ya mkuu wa mkoa na msafara wake kufika nyumbani kwa marehemu walikuta mke wa marehemu amefunga mlango na kuondoka na hakukuwa na hata mtoto nyumbani kwake.
Mke wa marehemu aliacha ujumbe kwa majirani kuwa hawezi kuwasubiri viongozi wa ccm kwani tangu marehemu mume wake amefariki hakuwahi kumwona huyo mkuu wa mkoa wala kiongozi yeyote wa ccm akifika nyumbani kwake kumtembelea.
ila anawaonaga tu madiwani na mbunge ambao wote ni kutoka chadema wakifika mara kwa mara kumtembele.
kituko kingine ni baada ya mkuu wa mkoa kufika uwanjani kuzindua kampeni na kujikuta anawahutubia wale aliokuja nao kutoka Arusha huku wenyeji wa kitongoji cha mwakey wakiwa wapo tisa tu na wa vijiji vingine kama watu kumi na tano tu.