Mkuu wa Mkoa unashindwa vipi!?

Kabulala

JF-Expert Member
Oct 13, 2019
695
935
Katika KAZI rahisi Sana ktk nchi hii mojawapo ni mkuu wa Mkoa (mwakilishi wa Rais kama wanavyopenda kujiita).

KAZI kubwa ya RC ni kusimamia ulinzi na usalama Kwa kupitia vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo mkoani kwake.

Kwangu Mimi hii ndio KAZI mama ya RC, Mambo mengine kama vile kuhamasisha maendeleo ni KAZI za ziada ,baada ya kuimarisha utulivu na Amani mikoani kwao. SASA kuna baadhi ya wakuu wa mikoa wanageuka kuwa wataalamu wa manunuzi, elimu, mahesabu,Afya, ujenzi n.k ktk maeneo Yao kitu ambacho sio kweli na matokeo yake wanaishia kukwaruzana na watumishi wao mikoani.

Nawashauri wasifanye KAZI zao kuwa Ngumu, wanapewa wataalamu wa kutosha na nyenzo nyingi kama hizo, wawatumie wataalamu hao ktk kutoa ushauri na maagizo pale tuu wanapobaini kuna uzembe binafsi. Lakini wakiendelea kujua kila Jambo sidhani kama watakua wanasaidia maeneo Yao.

Kwa kumbukumbu zangu za hivi karibuni sijawahi sikia wananchi wa Mkoa Fulani wakimsifia Sana RC wao Kwa maendeleo makubwa aliyowaletea, zamani wakuu wa mikoa walisifiwa Sana na wananchi Kwa kufanya mageuzi makubwa Sana ktk Nyanja mbali mbali kama vile kilimo na mifugo Kwa kutoa ushauri na kuhamasisha wananchi,but siku hizi wanashindana ni Nani ame upload clips nyingi YOUTUBE.

Mkuu wa mkoa inakubidi uwe symbol ya Rais haswa, ukienda ziara watumishi wanajipanga, sio kila kukicha wewe unaingilia vichochoro Hadi unaanza kugombana na mafundi (wakandarasi) site na wakati Una wataalamu kibao wanalipwa Kwa KAZI hizo.

Nazishauri media houses pia kuacha tabia za kuendekeza episodes za attention seekers, sioni logic za watu wa media kuwafuata nyuma viongozi wasio na jambo jipya na kubwa la kimageuzi kila waendapo kutimiza wajibu wao wa kawaida kama vile kukagua mitaro na vibanda vya wachuuzi..that way mtawachallenge waje na bigger ideas za kimageuzi zinazostahili coverage kwenye platforms zenu.
 
Hapo umesema kweli, Wakuu wa mikoa wengine wanajipa taabu za bure, wengine wagombana mpaka na wenyeviti wa ccm. Hawajui kutumia nafasi zao hao. Ndo maana wakitumbuliwa au kustaafu wanachoka akili na mwili kama walimu wa watoto tahira.
 
Hizo zote ni kwa sababu wawe talk of the town. Media Media Media.
Very right..but it is the shame Mwakilishi wa Rais kila siku Yuko vichochoroni na msururu wa YouTubers anahangaika na petty issues instead ya kuibuka na bigger ideas zinazoweza Kuleta maendeleo ktk jamii unayoiongoza..I swear to God najua siwezi kuteuliwa ata level ya Kijiji but where's the pride of being the Entire Region chief/incharge if there is no etiquette.
 
Hapo umesema kweli, Wakuu wa mikoa wengine wanajipa taabu za bure, wengine wagombana mpaka na wenyeviti wa ccm. Hawajui kutumia nafasi zao hao. Ndo maana wakitumbuliwa au kustaafu wanachoka akili na mwili kama walimu wa watoto tahira.
Very true.. yaani unakuta mkuu wa Mkoa anahangaika na miradi inayosimamiwa na wizara kama ya maji, kuna full expertise kila angle na Waziri mhusika ana full progress ya project. RC anazunguka pale na camera kila kukicha badala ya kukaa na wataalamu wake wa kilimo,uvivu, mifugo na kubuni miradi ya kusaidia wananchi.. Viongozi wetu wanasahau kwamba wanapewa vitendea KAZI Bora kama vile office nzuri,mishahara Safi na magari comfortable na dereva juu ili watumie comfort hiyo kufikiria namna ya kusaidia wananchi but do they do it?!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom