Mkuu wa Mkoa Mara -Mikutano ya siasa isiyomuunga mkono Rais katika maendeleo marufuku!

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,951
29,533
Mheshimiwa mkuu wa mkoa wa Mara aka kanda maalumu amepiga marufuku mikutano ya kisiasa isiyo na tija katika jitihada za maendeleo zilizoanzishwa na Rais Magufuli.

Mheshimiwa Mlingwa ameyesama haya wakati akipokea taarifa ya uchaguzu mkuu 2015 kutoka NEC.Ambapo imeonekana amani ya Mara imeimarika kiasi cha kuanza kuvutia wawekezaji!

Chadema kama mnataka kuwa na mkutano basi mkutano huo uhusiane na juhudi za Rais za kupambana na rushwa,kutengeneza madawati au mambo muhimu ya maendeleo kwa Taifa...sio mkutano wa kuelezea sababu za kumsusia Tulia.

Kwa habari zaidi source ni Itv
 
Unataka kusema tu kama kasuku??
Tunataka useme kwa mustakabali wa maendeleo ya Taifa
Unaujua huo mustakabali wa maendeleo ya Taifa??Taifa haliwezi kuongozwa na fikra za mtu mmoja,lazima mawazo mbadala yatolewe!Hii kufata mkumbo bila kuhoji haina afya kwa Taifa!Katiba ndio muongozo mkuu wa nchi,katiba imetoa uhuru wa kujieleza!
"Ukiona kiongozi anavunja katiba,hata kama huyo kiongozi ni mzuri hatufai"-By Nyerere
 
Mawazo mbadala yalenge maendeleo sio matusi au kujijenga kisiasa
 
Mawazo mbadala yalenge maendeleo sio matusi au kujijenga kisiasa
Kuna vyombo vinavyoshughulika iwapo kutatokea uvunjifu wa sheria!Moja ya malengo ya vyama vya siasa ni kushika dola,suala la kujijenga kisiasa halikwepeki!
Vyama vya upinzani vitakosoa tu,hata kama hupendi ndio hivyo!Yaani uitishe mkutano kwa ajili ya kusifia,hell no!Kosoa ili watu watimize wajibu wao
 
Safi sana hawa ndio aina ya viongozi tunaowahitaji kwa sasa huu ni mda wa kazi sio majungu na kumkwamisha Rais asifanye kazi.
Lowassa hoyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee hoyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee hoyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee hoyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Unaujua huo mustakabali wa maendeleo ya Taifa??Taifa haliwezi kuongozwa na fikra za mtu mmoja,lazima mawazo mbadala yatolewe!Hii kufata mkumbo bila kuhoji haina afya kwa Taifa!Katiba ndio muongozo mkuu wa nchi,katiba imetoa uhuru wa kujieleza!
"Ukiona kiongozi anavunja katiba,hata kama huyo kiongozi ni mzuri hatufai"-By Nyerere
Ila bro serikali ya awamu ya tano imefanya makubwa na imejtahid sana wala co yakubezwa kwa maana sukari huku kwetu dar ni 1800, cement ni 8000 alaf wala kodi za benki sisi hazituhusu alaf na ile kodi ya 1000 kwa mwezi ya laini za simu pia haipo.. Ccm mbele kwa mbele #nchiyamwendokasi
 
Mawazo mbadala yalenge maendeleo sio matusi au kujijenga kisiasa
kwani kazi ya mwanasiasa nini? .kama siyo kujijenga? na kwa taarifa yako magufuli anacho kifanya ni kujiimarisha kisiasa.
 
Mwaka huu MNA Kazi kwelikweli njia rahisi in kuvifuta vyama vya upinzani ibaki ccm ilete maendeleo licha ya kupambana miaka 50 bila kufanikiwa
 
Back
Top Bottom