Mkuu wa Mkoa Mara awasimamisha maafisa elimu sita

mgeni wenu

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
3,664
1,730
Mkuu wa mkoa wa Mara Bw. Magesa Mulongo ameagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa maafisa elimu wa halmashauri sita za mkoa wa Mara huku Wakurugenzi Watendaji wa halmashauri hizo wakitakiwa kujieleza baada ya kushindwa kutoa zawadi za watumishi bora wa idara ya elimu kwa mwaka mmoja hadi miwili hatua ambayo amesema inachangia kushusha ari ya utendaji wa kazi kwa watumishi hao.
 
Fungu la zawadi lilikuwepo? Isije kuwa hakukuwa na fungu, sasa hapo wangetoa zawadi kutoka katika fungu lipi?
 
Kazi kweli kweli,sijui kama kuna fungu la zawadi kwa halmashauri,kama lipo wamekula,sawa kama halipo kuna tatizo hapa,lakini wengine wageni wana mwaka mmoja tu
 
Kumsimamisha mtu kazi ni kupisha uchunguzi. Sasa hapo kuna uchunguzi gani zaidi ya kutaka Maelezo toka kwa wahusika? Sasa hivi kazi za watu haziheshimiwi kama watu wanavyoziheshimu ajira zao. Huu mtindo mkeo akikunyima humo nyumbani unaenda kusimamisha watu kazi utafanya watu badala ya kufanya kazi kwa moyo watafanya kwa mshahara tuu
 
Huyu bwana akili zake nafikiri yafaa wataalamu wafungue hiyo kichwa na kuangalia kama hazina matatizo
 
Sababu zingine za kiboya aisee kufukuzana, waalim wenzang na mm wa mahesabu hakikisheni mnasolve swali ubaoni mpaka liishe, ukiliacha linahang unaweza kukuta mkuu wa wilaya mwenye taaluma ya mashairi anakupga chini
 
#Habari:Mkuu wa mkoa wa Mara Bw.Magesa Mulongo ameagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa maafisa elimu wa halmashauri sita za mkoa wa Mara huku Wakurugenzi Watendaji wa halmashauri hizo wakitakiwa kujieleza baada ya kushindwa kutoa zawadi za watumishi bora wa idara ya elimu kwa mwaka mmoja hadi miwili hatua ambayo amesema inachangia kushusha ari ya utendaji wa kazi kwa watumishi hao.
Kwani lazima wawepo wafanya bora kila idara? Kama wote wameboronga watawapaje zawadi? RC tumieni akili kidogo siyo kusimamisha simamisha watumishi ovyo.
 
MMhhhhh kama ni kweli kafanya hivi basi tuna safari ndefu sana ya kutambua maana ya utawala bora! Yani siku hizi kila kitu ni amri amri tu. Simamisha hapa, fukuza pale, Fokea kule.Kazi za umma jamani zina utaratibu wake, ni muhimu ukazingatiwa. Huwezi kuendesha kazi za umma kama za crocery yako.
 
Zawadi?huyu Mkuu wa mkoa atatumbuliwa muda si mrefu ,acha amtengenezee polepole njia ya kuwa mkuu wa mkoa soon
 
aliyesimamishwa jamani ni mmoja na sio sita kama mleta taarifa, kwanza alitoa sababu za uongo, na hata washindi wa mwaka wa jana hawakupewa hela alivyoulizwa akawa hana majibu anatumbua tu macho.. ndipo akaagiza asimamishwe. ila wengine wameambiwa wahakikishe hadi kesho saa 8 wanawapa wafanyakazi bora stahiki zao. msioelewa bora mkae tu kimya hizo hela watu wanazipiga kwa juu...
 
Angali page ya Itv imesemaje,maana ndo page ya Television ya taifa yenye vision
 
Kama hakuna watumishi waliofanya vizuri kwenye idara ya elimu, wapewe tuu? Gadeem
 
Kuna kama ka dalili za kuchanganyikiwa hivi! ngoja tusubiri; Zawadi za waalimu zinatolewa na shule husika na sio Mkurugenzi wala Afisa Elimu! Baada ya mpango wa elimu bure hakuna michango shuleni, na Pesa za Magu zinakuja na maelekezo ya matumizi, hakuna fungu la zawadi wala hongera. labda shule iwe na miradi binafsi kama kufuga nguruwe!

Kwa nini watumbua majipu hawaulizi kwanza kabla ya maamuzi?
 
Naamini zawadi kama hizo hutolewa baada ya wadau kufikia vigezo fulani walizojiwejea.
Kama hakuna aliyefikia vigezo maana yake zawadi haitoki ndio maana ushiriki wa competition yeyote mwisho wanasema vigezo na masharti kuzingatiw
 
Back
Top Bottom