Mkuu wa Mkoa anusurika kuzama Ziwa Tanganyika

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Fadhili Abdallah

MKUU wa Mkoa wa Kigoma, Joseph Simbakalia ameonja adha ya kutokuwepo kwa barabara kuelekea katika vijiji vilivyopo mwambao wa ziwa Tanganyika baada ya kunusurika kuzama na boti ziwani mara mbili kufuatia boti aliyokuwa akisafiria kupigwa na mawimbi mazito.

Simbakalia ambaye alikuwa akiendelea na ziara ya kukagua miradi ya maendeleo mkoani
humo kwa mara ya kwanza alikumbana na wimbi wakati akielekea katika kijiji cha Kagunga,
mwambao wa Kaskazini wa ziwa Tanganyika kukagua ujenzi wa soko la mpakani ambapo boti
aliyokuwepo ilipigwa na wimbi zito na kufanya watu wote waliokuwepo kwenye boti hiyo
kuloana chapa chapa.

Baada ya misukosuko ya siku hiyo Mkuu wa Mkoa Kigoma na msafara wake walifanikiwa kurudi
salama mjini Kigoma na siku iliyofuata alikuwa akiendelea na ziara katika vijiji vya mwambao wa kusini wa Ziwa Tanganyika.

Ni katika eneo hilo la milima ya Hifadhi ya Taifa ya Mahale wakati akielekea kijiji cha Kalya kilometa 24 kutoka makao makuu ya hifadhi, msafara wa Mkuu huyo wa mkoa ilipata dhoruba kubwa ambapo wakati hali hiyo ikiendelea walimshauri nahodha wa boti waliyopanda atafute mahali pa kujificha ili kuepukana na dhahama hiyo.

Hata hivyo, jambo hilo halikuwezekana kutokana na eneo ambalo boti hiyo ilikuwa imefikia
kuwa na milima na miamba ambayo hairuhusu boti kuegeshwa wakati wa mawimbi makubwa na hivyo kulazimu safari ya kifo kuendelea.

Pamoja na Mkuu wa Mkoa Kigoma katika msafara huo pia alikuwemo pia Mkuu wa wilaya
Kigoma, John Mongela, kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya, Meneja ujirani mwema wa Shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA), waandishi wa habari watatu na Ofisa Tarafa wa Buhingu, Omari Kiembe.

Mwandishi wa habari hii ambaye alikuwa mmoja wa abiria katika boti hiyo alishuhudia
msukosuko huo ambao ulichukua takribani saa mbili hali ambayo iliwafanya abiria waliokuwa ndani ya boti hiyo kila mmoja kwa imani yake kuomba Mungu awanusuru.

Kwa mujibu wa wakazi wa eneo hilo walieleza kuwa mawimbi ambayo mkuu wa mkoa na msafara wake walikutana nayo yanajulikana kama Lukuga ikiwa ni asili ya upepo kutoka mto Lukuga nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) ambayo unaingia ziwani katika eneo hilo.

Pamoja na misukosuko hiyo Mungu aliibariki safari hiyo ya mkuu wa mkoa na kufanikiwa kufika salama katika kijiji cha Kalya ikiwa ni mara ya kwanza kwa mkuu huyo wa mkoa kufanya
ziara katika eneo hilo.
 
Simbakalia nakupa pole, shirikiana vyema na wabunge na wananchi wako ili muendeleze mkoa wenu.
 
hapana hawa ni watendaji wazuri sana na raia wema wa nchi hii tena wapambanaji, kwa nini uwaombee vifo? hay andio ninayoyasema huyu invicible kashindwa kazi
 
Back
Top Bottom