Eti mkuu wa mkoa amechukua nafasi ya Bilionea Reginald Mengi.?
Inaingaia akilini kweli?
Ana viwanda vingapi?
Ana makampuni mangapi?
Huyo huyo bwana mkubwa alitumika sana kumshambulia Mzee Lowasa aliyekitumikia Chama ,Jeshi ,Ukurugenzi wa AICC ,Ubunge ,uwaziri mpaka Uwaziri mkuu kuwa ni Fisadi anawahonga viongozi wa Dini na haijulikani anapata wapi pesa ?
Wakati huo huo ni wazi kuwa Lowasa alitokea Familia tajiri kwa mifugo na pia alitumikia taifa hili kwa muda mrefu.
Lakini bado wakina Pole pole,Membe, Nape, Dr.Slaa ,Lisu, Kubenea na wengine walitumia Muda mwingi kumshambia na kumuita fisadi mpaka CCM ikamkata na kumweka MTU waliyeamini atakomesha tabia ya Watawala kutumia ofisi za umma kujilimbikizia pesa kutoka kwa matajiri bila kueleza wanapewa mapesa hayo ili nini na kwa faida ya nini wakati nchi ina madeni makubwa na umaskini mkubwa.
Kama Serikali inaruhusu wakuu wa mikoa wana miliki mpaka Timu za Mpira kama Bilionea Mo. Watuambie hii nchi ni ya Kijamaa au Kibepari tena sio ubepari ule wa unaotambulika kikatiba kama kule marekani Bali ubepari wa kutumia ofisi kujitajirisha bila kuwa na biashara inayojulikana wazi.
Wakati huo huo wanashanga mzunguko wa pesa unakua mdogo kumbe kuna watu wanatumia pesa nyingi kutoka kwa wafanyabiashara kwa ajili ya kufanya kampeni za kujipaisha kisiasa.
Mkuu wa mkoa anatafuta umaarufu ili iweje wakati nchi yetu wakuu wa Mikoa hawapigiwi kura zaidi ya kuteuliwa.
Mara vikao na viongozi wa dini, Mara wasanii ,Mara zawadi za magari binafsi kwa polisi wakati kuna vituo havina hata pikipiki.
Haya yanafanyika ili iweje?
Kama kila mkuu wa Taasisi akianza kukusanya watu kwenye makumbi kwa gharama zake itakuaje?
Kuna kazi itafanyika kweli ?
Siamini kuwa huyo MTU ndiye peke yake ametawala mkoa kuliko wengine wote waliopita na hawakuwa na mapesa ya kugawa kama huyo.
Awamu hii inatengeneza watu watakaoisumbua sana nchi kuelekea 2530 wakati wa kinyanganyiro.
Kuna makundi makubwa na mabaya yataibuka ndani ya CCM kuliko wakati wowote mana yatakua ni makundi pendwa dhidi ya makundi yanayoonekana hayastahili hata kuishi duniani.
Khatari sana !!
Ndio maana wengi wanabaki kishangaa kuwa huo ufisadi na matumizi mabaya ya ofisi unaotajwa ni upi?
Tukitaka kujenga taifa zuri kwa muda wote ni lazima tuweze kukataa aina zote za matumizi mabaya ya ofisi kwa manufaa binafsi.
Wengine wakifanya hovyo wataanza kusakamwa na wale wanaowapa hayo mapesa watakamatwa na kuitwa wahujumu uchumi.
Huyu je ,anapewa na nani na kwa nini isiwe ni waziri kwenye dhamana ,tena mwenye bajeti kubwa na miradi ambayo anaweza kujitetea.
Hii nchi inasikitisha sana hasa awamu hii tuliyokuwa tumeiamini sana.
Kama mkuu wa mkoa anaweza kuchangisha mapesa anavyotaka yeye bila kuulizwa wala kuzuiliwa itakuaje kwa waziri?
Hivi mfano Waziri Mkuu au Waziri wa Fedha au waziri wa mambo ya ndani au waziri wa Tamisemi au waziri wa Ardhi wote hao kwa mfano wakikosa uadilifu kama alivyo mkuu wa mkoa wakaamua kuchangiasha mapesa kimya kimya kutoka kwa matajiri wasiojulikana itakuaje?
Bora hata Lowasa alikua anachangisha kwa uwazi lakini hao hao akina Polepole walisema anaomba mwenyewe kuitwa kwenye matamasha na Harambee ili apate umaarufu wa kisiasa.
Leo wakati nchi ikiwa kwenye kipindi wanachokiita cha mpito cha wanyonge kufungwa mikanda watawala wanagawa magari na mapesa wanavyotaka.
Khatari sana !!
2020 nitashangaa mtu huyo aliyetumia muda wa miaka mitano kutoa rushwa akipewa nafasi ya kugombea hata udiwani.
Nategemea kuona anakatwa mana ametumia pesa kujipa kiki tena akiwa kwenye ofisi ya umma.
Hivi haoni kuwa anatengeneza genge la wafanyabiashara ambao baadae akija kiongozi mwingine mwenye visasi na vinyongo , wataanza kuandamwa na kujikuta wanapata misukosuko ya kibiashara?
Ili huyo MTU ajitambue na kuwa na uchungu na Taifa hili ni vizuri akawekwa pembeni ili ajifunze kuwa hii nchi ni maskini. Tunahitaji mipango mikubwa ya kiuchumi sio siasa na kujijengea umaarufu.
Wanapenda Ufahari,ubepari kama Maseneta wa Marekani wakati nchi ni maskini na wao wenye we hawana biashara wala viwanda vya kwao na familia zao zaidi ya madaraka na ofisi wanazozitumia kuwashurutisha wafanyabiashara amaboa wanakuwa waoga kutokana na imani iliyopo kuwa huyo MTU hagusiki na analindwa na mkubwa wa nchi.
Siamini kuwa kama kweli wanamuenzi Mwalimu Nyerere wangeyafanya hayo wakati akiwa hai.
Wanayafanya mana hakuna wa kukemea. Nchi ina watwala wa kujenga hofu kwa watu kutumia dola na watu kama akina Msiba mkuu badala ya kujenga maadili ya uongozi ambayo kwa hakika yamepotea kabisa awamu hii. Awamu inayowaminya wapinzani , wafanyakazi,wafanyabiashara tuu ,huku watawala wakiwa wanalewa madaraka alimradi wajionyeshe kuwa wanawachukia wafanyakazi ,wafanyabiashara na wapinzani.
Yani MTU akionyesha hayo anaweza akapiga hata mtu panga bila kuulizwa.
Mfano ni Mchochezi wa mauaji Msiba mkuu. Hakamatwi wala hahojiwi kisa anasema yeye ni mshaniki wa kuunga mkono juhudi.
Khatari sana.