Ninachosema ni kuwa Mkuu wa majeshi ni lazima afahamu mipaka yake ya kikaziKatiba iheshimiwe na watu wote, machafuko ya ndani kwenye nchi nyingi mara nyingi huwa yanaletwa na watawala kutofuata katiba.
Tunajua kuwa Katiba ya nchi inampiga marufuku Mkuu wa majeshi nchini, kujiingiza kwenye mambo ya kisiasasometimes ukiwatisha watu unawafanya wajipange na kuwa aggressive zaidi. ni reaction ya kawaida ya wanyama na binadamu.
Hivi sirro ni msukusu?Tofauti ya msukuma n'a cow ni pembe na mkia.. Ukistaajabu ya meko na sirrro utayaona ya mobeyo
Sent using Jamii Forums mobile app
Maneno yote na hali ilivyo sasa nchini kwetu ameieleza vizuri katibu mkuu wa ccm ndugu bashiri hao waliobakia ni ma yoyo yo tu.Katiba iheshimiwe na watu wote, machafuko ya ndani kwenye nchi nyingi mara nyingi huwa yanaletwa na watawala kutofuata katiba.
Jamaa kaona NDIYOOOO hazitoshi sasa anazisaka hasa, yaani kama hutaki kusema NDIYOOOO basi nyamaza, la sivyo utaitwa mchochezi.Tunajua kuwa Katiba ya nchi inampiga marufuku Mkuu wa majeshi nchini, kujiingiza kwenye mambo ya kisiasa
Kama yeye Venance Mabeyo "anatamani" kuwa mwanasisa, tunamwomba kwanza avue magwanda yetu ya Jeshi, ili avae nguo za kijani, ili aweze kupambana katika ulingo wa kisiasa
Jamaa kaona NDIYOOOO hazitoshi sasa anazisaka hasa, yaani kama hutaki kusema NDIYOOOO basi nyamaza, la sivyo utaitwa mchochezi.
Kwanza toka lini mwanajeshi akamkamata raia kwasabu ya kauli tu?
Mbona tunaona mara kwa mara Wasomali wanachaniza tu mipakani?
Kwani yeye peke take? Uongozi wote wa nchi yetu umeweka Katiba na sheria zote pembeni na kuongoza kwa amri na maagizo toka juu. Ni Awamu ya mipango, mikakati na michakato ya mikutanoni, kwenye semina na makongamano wananchi wakiachwa na matatizo yao wakitakiwa kuwa wazalendo na wapende nchi yao.Tumemsikia wenyewe kwa masikio yetu, mkuu wa majeshi nchini, Venance Mabeyo, akiwapiga mkwara watanzania, kuwa wao kama Jeshi la wananchi nchini, wanafuatilia kwa karibu kile alichokiita kuwa ni kauli za kichochezi zenye nia ya kuleta machafuko nchini
Kwanza lazima tuelewe wajibu wa Jeshi la wananchi nchini
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977, ibara ya 147(3) imesema wazi kuwa itakuwa marufuku kwa mwanajeshi yeyote kujiunga na chama chochote cha siasa nchini, na jukumu lao kubwa ni kulinda mipaka ya nchi yetu, kuhakikisha kuwa hatuvamiwi na nchi yeyote jirani. Mwisho wa kunukuu
Katiba ya nchi inasema wazi kuwa mwanajeshi yeyote hatakiwi kujiunga na chama chochote cha kisiasa na imeeleza kuwa wajibu wao mkubwa ni kulinda mipaka ya nchi yetu ili tusivamiwe. Sasa nilichokisikia kutoka kwa mkuu wa majeshi ndiyo wajibu wake kikatiba??
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,ya mwaka 1977, ibara ya 18(1) inaeleza wazi kuwa kila mwananchi yuko huru kutoa maoni yake, kuhusiana na uendeshaji wa nchi yake
Katiba hiyo hiyo ya nchi imeeleza wazi kuwa chombo pekee cha kutafsiri sheria ni mahakama na ndiyo wanaoweza kusema kuwa kauli iliyotolewa na mwanasiasa fulani ni ya kichochezi au laa
Sasa kwa Mkuu wa majeshi nchini kupiga mkwara mzito kuwa eti Jeshi lake halitavumilia kauli yoyote ya kichochezi, siyo kuivunja Katiba ya nchi waziwazi na kuingilia mhimiki wa mahakama kiutendaji??
Wao wanajeshi wanapaswa wabaki (barracks) na wajibu wao mkubwa ni kulinda mipaka ya nchi yetu na hawapaswi hata kidogo kuingilia mambo ya kisiasa nchini, kwa kuwa kwa kufanya hivyo watakuwa wanataka kuleta machafuko nchini
Mungu ibariki Tanzania
Tatizo la nchi yetu hii ni siasa. Hata wasiotakiwa kufanya siasa nao hujiingiza ktk siasa.Tunajua kuwa Katiba ya nchi inampiga marufuku Mkuu wa majeshi nchini, kujiingiza kwenye mambo ya kisiasa
Kama yeye Venance Mabeyo "anatamani" kuwa mwanasiasa, tunamwomba kwanza avue magwanda yetu ya Jeshi, ili avae nguo za kijani, ili aweze kupambana katika ulingo wa kisiasa
Absolutely trueHizo kauli za vitisho kabla ya kuzitoa aangalie nyakati,ile nadharia ya kuamini watz ni waoga wajinga waitafakari mara Mbili Mbili. Salama yao si vifaru wa mabomu hayo huwa mazito kuyatumia wakati ukifika, Salama yao iko kwenye kutenda haki kwa walipa kodi.Wakidhani wana nguvu kuliko umma wajitafakari.Gadafi ,Bashiru, Mugabe nk waliwekeza kwenye jeshi na hali kuwasaidia.Upepo wa Sudan utafika utakuja tu Africa Mashariki watafute makaravati ya kujifichia kama wataendelea kutenda dhuluma.
Hivi huyu Jenerali Mabeyo anaisoma kweli hii Katiba yetu ya nchi??