Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,477
- 30,130
Tumemsikia wenyewe kwa masikio yetu, mkuu wa majeshi nchini, Venance Mabeyo, akiwapiga mkwara watanzania, kuwa wao kama Jeshi la wananchi nchini, wanafuatilia kwa karibu kile alichokiita kuwa ni kauli za kichochezi zenye nia ya kuleta machafuko nchini
Wajibu wa Jeshi la Wananchi nchini
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977, ibara ya 147(3) imesema wazi kuwa itakuwa marufuku kwa mwanajeshi yeyote kujiunga na chama chochote cha siasa nchini, na jukumu lao kubwa ni kulinda mipaka ya nchi yetu, kuhakikisha kuwa hatuvamiwi na nchi yeyote jirani. Mwisho wa kunukuu
Katiba ya nchi inasema wazi kuwa mwanajeshi yeyote hatakiwi kujiunga na chama chochote cha kisiasa na imeeleza kuwa wajibu wao mkubwa ni kulinda mipaka ya nchi yetu ili tusivamiwe. Sasa nilichokisikia kutoka kwa mkuu wa majeshi ndiyo wajibu wake kikatiba??
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,ya mwaka 1977, ibara ya 18(1) inaeleza wazi kuwa kila mwananchi yuko huru kutoa maoni yake, kuhusiana na uendeshaji wa nchi yake
Katiba hiyo hiyo ya nchi imeeleza wazi kuwa chombo pekee cha kutafsiri sheria ni mahakama na ndiyo wanaoweza kusema kuwa kauli iliyotolewa na mwanasiasa fulani ni ya kichochezi au laa
Sasa, kwa Mkuu wa majeshi nchini kupiga mkwara mzito kuwa eti Jeshi lake halitavumilia kauli yoyote ya kichochezi, siyo kuivunja Katiba ya nchi waziwazi na kuingilia mhimili wa mahakama kiutendaji?
Wao wanajeshi wanapaswa wabaki (barracks) na wajibu wao mkubwa ni kulinda mipaka ya nchi yetu na hawapaswi hata kidogo kuingilia mambo ya kisiasa nchini, kwa kuwa kwa kufanya hivyo watakuwa wanataka kuleta machafuko nchini.
Mungu ibariki Tanzania