Mkuu wa Kituo cha Trafiki Luguruni ndugu Magembe

Verily Verily

Senior Member
Jan 4, 2007
192
148
1. Huyu mtu anategeshea magari yanayowahi kazini kabla ya saa 12:00 na kuyakamata kwa makosa ya kipuuzi

2. Anaweka lock up madereva kituoni zaidi ya masaa 10 bila sababu ya msingi na hivyo waliokamatwa kukosa kwenda kazini siku hio na kuwasababishia watanzania kukosa huduma maofisini.

3. Madereva hasa wa bodaboda na hata wa magari wakitolewa lock up ni kulipa faini bila kupewa risiti.

4. Anasababisha foleni barabara ya Kimara hasa wakati wa alfajiri watu wanapokuwa wanawahi makazini kwa kuzuia matumizi ya lane mbili ambazo upana wa barabara unaruhusu. Hata lori likiharibika lazima kulisubiri.

5. Mamlaka husika zisimwache mtu huyu kufanya atakavyo. Ni hatari kwa ustawi wa nchi.
 
Ulicho sema ndugu nikweli kabisa hata me ni muhanga wa huyo jamaa,na wakati mnaachiwa anajisifu kwamba lolote utakalo mwombe baya kwakuwa amekuweka lupango halita mkuta yy anatenda lililo haki,chakujiuliza magari yakikaa line moja yatafika saa ngapi maofisini?na kwanini wakiwa wanakuweka ndani hawakupi nafasi ya kujieleza?sheria inasema ulipie fine au upelekwe mahakamani uhukumiwe kwa kadiri ya makosa uliyo yafanya yy hafanyi hivyo.
 
Ajabu nyingine ni kuto kutumia mashine za TRA walizopewa na serekali kukusanyia mapato ya serekali.Notification wanayo itoa ni ya mwaka 2011,sasa sijui masijala ya serekali inatumia vitabu vilivyokwisha muda wake?
 
Piga simu trafiki kitengo cha malalamiko au Mpinga direct. Kitu muhimu ni kwa trafiki kutengeneza njia kwa magari madogo kupita kuwahi kazini
 
Piga simu trafiki kitengo cha malalamiko au Mpinga direct. Kitu muhimu ni kwa trafiki kutengeneza njia kwa magari madogo kupita kuwahi kazini

Hebu weka namba ya Afande Mpinga hapa wahanga wa huyu "mfalme wa Kimara" tuwasiliane na bosi wake.

Jambo baya kabisa kabisa ni kuchukua pesa bila risiti na EFD machine zikiwa zipo kituoni na kuonekana waziwazi
 
hapo kosa ni kutokutoa risiti tu.hayo mengine yuko sahihi kabisa..haiwezekan mtu uvunje sheria makusudi uachwe eti Kisa unawahi ofisini.
 
hapo kosa ni kutokutoa risiti tu.hayo mengine yuko sahihi kabisa..haiwezekan mtu uvunje sheria makusudi uachwe eti Kisa unawahi ofisini.

Exactly brother, ahukumiwe kwa kuibia serikali, actually Takukuru inahusika moja kwa moja.
 
Uchunguzi ufanyike kama ni kweli hatua zichukuliwe dhidi yke hakuna mwenye mamlaka zaidi ya kufuata sheria,wahusika fatualieni lalamiko hili,ngazi za juu
 
Uchunguzi ufanyike kama ni kweli hatua zichukuliwe dhidi yke hakuna mwenye mamlaka zaidi ya kufuata sheria,wahusika fatualieni lalamiko hili,ngazi za juu

Lakini sio mara ya kwanza huyu "mfalme" analalamikiwa. Labda safari hii kilio kitasikilizwa
 
Nizaidi ya jipu na wanamchezo mchafu sana wanamweka askari 1 pale kwa msuguri kwenye kona anawaonyesha mpite pembeni ukifika mbele unakamatwa. Alituweka lokup bila kujieleza huyo jamaa jioni anajisifu tukawe mabalozi wazuri duh!ngachoka kabsaaaa
 
Nizaidi ya jipu na wanamchezo mchafu sana wanamweka askari 1 pale kwa msuguri kwenye kona anawaonyesha mpite pembeni ukifika mbele unakamatwa. Alituweka lokup bila kujieleza huyo jamaa jioni anajisifu tukawe mabalozi wazuri duh!ngachoka kabsaaaa[/QUOTE

Vipi tupeni mrejesho
 
Back
Top Bottom