Mkuu wa Jeshi la Polisi wa tatu, IGP Mstaafu Samweli Huma Pundugu afariki dunia

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
1.jpg
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARl KUHUSU KIFO CHAIGP MSTAAFU SAMUEL H.PUNDUGU

lnspekta Jcnerali wa Polisi anasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa lnspkta Jenerali wa Polisi Samweli Huma Pundugu aliyefariki tarehe 26".09.2018 jijini Dar es Salaam.

IGP Mstaafu Pundugu aliyezaliwa mwaka 1928 aliteuliwa kuwa Inspekta Jenerali wa Polisi mwaka 1973 akiwa ni Mkuu wa Jeshl la Polisi wa tatu na aliliongoza Jeshi hilo hadi mwaka 1975. Kabla ya uteuzi huo alikuwa akifanya kazi Makao Makuu yn Polisi kama Mkuu wa kitengo cha Oparesheni na Mafunzo akiwa na cheo cha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP).

IGP Mstaafu Pundugu, alijiunga na Jeshi la Palisi mwaka 1948 baada ya kumaliza shule ya Sekondari ya Wavulana ya Tabora (Tabora Boys) na alipata ajira rasmi mwaka 1949.

Banda ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Jeshi la Palisi, IGP Mstaafu Pundugu , allbadilisha uongozi wa Chuo cha Palisi Moshi na Kamishcni ya Upelelczi kuongozwa na Kamishna wa Palisi (CP) tofauti na alivyokuta nafasi hizo zilizokuwa zikiongozwa na Makamishna Wasaldizi Waandamizi (SACP's).
Mwaka 1964, akiwa Afisa wa Jeshi la Palisi kabla ya kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Mstaafu Pundugu aliteuliwa kwenda Zanzibar kumsaidia Kamishna Wa Jeshi la Polisi aliyeteuliwa kuongoza Jeshl la Palisi Zanzibar.

IGP Mstaafu Samuel Pundugu alikuwa ameweka msisitizo wa hali ya juu katika uongozi wake hususan katika eneo la nidhamu, usafi, utayari na ukakamavu wakati wote wa uongozi wake ili kuwezesha Jeshi la Polisi kufanya kazi kwa ufanisi.

Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Mji Mwema, Kigamboni jijini Dar es Salaam. Taarifa zaidi zitatolewa kadri mipango itakapokamilika

BWANA AMETOA ,BWANA AMETWAA , JINA LA BWANA LIHIMIDIWE. AMINA

Pamoja na msiba tulionaonao, bado tunasisitiza umuhimu wa wananchi kushiriki katika mapumbano
dhiidi ya uhalifu kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu.

Wananchi tuendelee kudumisha aman, umoja na Ushirikiano katika taifa letu.

UMOJA WETU NDIO NGUVU YETU.

1.jpg
 
Hawa ma Cop wa miaka hiyo walikuwa waadilifu na waliosimamia sheria na kanuni bila kuweka maslahi yao binafsi mbele,japo historia inaonyesha kuwa. "Kutumika"na wenye mamlaka hakujawahi kukwepeka lakini angalau walikuwa wanastahili kweli kuitwa maaskari! Rip afande
 
Hawa ma Cop wa miaka hiyo walikuwa waadilifu na waliosimamia sheria na kanuni bila kuweka maslahi yao binafsi mbele,japo historia inaonyesha kuwa. "Kutumika"na wenye mamlaka hakujawahi kukwepeka lakini angalau walikuwa wanastahili kweli kuitwa maaskari! Rip afande
Je hawa vodafasta wa sasa ? Rushwa mbele na matumizi ya nguvu bila busara.
 
Imekuwa aje mtumishi wa kipindi cha nyuma kiasi hiki kutolewa taarifa?
 
Back
Top Bottom