Mkuu wa Chuo CBE fuatilia matatizo haya

kipoke KIPOKE

Member
Apr 20, 2015
54
95
Sasa hivi kuna mitihani inaendelea, cha kushangaza vijana wetu baadhi wamelipa ada lakini hawajafanya mitihani kwa sababu mbalimbali za kichuo eti system. Wamepewa ratiba nyingine maana watafanya mitihani tofauti sasa kwa kasi hii matokeo ya wanafunzi darasa moja vipimo tofauti inasikitisha sana.

Kuna kastaili kengine eti wanaita kukata rufaa. Mwanachuo akifeli anaruhusiwa kukata rufaa kwa tshs 20,000/=kwa somo. Sina hesabu kamili ila ni pesa nyingi sana maana kozi moja ina wanafunzi zaidi ya 600 na kuna shift 2(night na full time).

Je ni shs ngapi basi zinapatikana wakati hata hizo barua hawafungui hakuna anayebadilishiwa matokeo maana hawafanyii kazi ni wizi mtupu. Haya inawezekanaje mwaka wa kwanza,wa pili na watatu kufanya mtihani unaofanana?

Aibu kwa wizara, Waziri fuatilia hili hii ni aibu kwako maana kipo chini yako.
Imekua kama shule ya awali (chekechea). Kwa sababu zao binafsi wanaahirisha mitihani bila kujali wala kushirikisha wanachuo wao na ratiba walitoa wenyewe.

Mkuu wa chuo hebu fuatilia mambo madogomadogo kama hayo .
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom