Sangarara
JF-Expert Member
- Sep 29, 2011
- 13,104
- 5,665
Club ya yanga inafanya mkutano wake na unarushwa live na clouds tv,huku nikiwapongeza kwa hilo naomba kuweka sawa baadhi ya mambo.
Kuna taarifa imetolewa na wote wawili mwenyekiti na makamu mwenyekiti kwamba timu ilipotembelea bungeni kupeleka kombe la kagame ilijipatia mapato ambayo yamekuwa classified kama mapato ya kibiashara jumla ya shiling 84M. Hapo mwanzo ndugu mwenyekiti alidai kwamba michango ya hiari iko classified kama grants lakini michango ambayo imeainishwa kwenye katiba ni mapato yanayojumuishwa na mapato ya kibiashara.
Hapa naona kama kuna upotoshaji wa makusudi unafanywa na ndugu mwenyekiti ili kuonyesha ufanisi wake katika kuanzisha vyanzo vya mapato vya kibiashara katika kipindi kifupi tu cha uongozi wake.
Kiasi cha shilingi 84M ni ahadi zilizotolewa na wabunge kwakwamba watakuwa wanachangia shilingi laki tano kila mwaka.
Lingine ni kwamba mwanasheria anayewapatia ushauri na huduma ya kisheria waliokuwa waajiriwa wa Yanga african watatu katika kesi dhidi ya yanga ambazo tayari mahakama imekwishakutoa hukumu dhidi ya yanga amevuliwa uanachama wake leo baada ya takribani wananchama wote kupiga kura ya ndio dhidi yake kwa madai kwamba hawezi kuendelea kuwa mwanachama wa yanga huku anasimamia kesi kadhaa dhidi yake.hii nayo imekaa vibaya.
Hivi sasa wanachama wanatoa mawazo yao juu ya uwekezaji kwenye jengo la mafia.